UJUE UGONJWA WA MARBURG UNAOFANANA NA EBOLA


UTANGULIZI
Tarehe 19 0ctober 2017 shirika la afya duniani (WHO) lilitoa taarifa kuhusu kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa MRBURG (MARBURG VIRUS DISEASE) katika nchi jirani ya UGANDA.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali ya UGANDA na shirika la Afya Duniani(WHO) mlipuko huo ulithibitishwa kwa kupitia vipimo vya maabara baada ya kutokea wagonjwa wane ambapo kati yao 3 walipoteza maisha.

Kwa kuzingatia kwamba nchi yetu inapakana nan chi ya Uganda,kutokana na mwingiliano wa watu na shughuli mabali mbaliza kijamii,upo uwezekano wa ugonjwa huu kuvuka mipaka na kuingia nchini kwetu.

NINI MAANA YA MARBURG
Marburg ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kitaalamu kama Marburg virus.
Ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kama homa ya virusi zinazosababisha kutoka damu sehemu za wazi za mwili mfano puani,masikioni,na machoni.
Huathiri binadamu na wanyama kama nyani,ngedele,sokwe na popo.
Ugonjwa huu usafiri kwa kasi na kusababisha vifo vya watu wengi.


NJIA ZA KUPATA MARBURG VIRUS.
Kutoka kwa mtu aliambukizwa au wanyama kwa:

 • Kugusa majimaji ya mwili toka kwa mtu aliyeambukizwa,mfano damu,matapishi,mkojo,jasho,mate,machozi na kamasi
 • Kugusa maiti ya mtu aliyefariki kwa ugonjwa wa Marburg
 • Kugusa godoro,shuka,blanket au nguo zilizotumiwa na mgonjwa wa Marburg
 • Kuchomwa na sindano au vifaa visivyo safi na salama
 • Kugusa mizoga au kula wanyama pori kama vile sokwe,nyani,na popo
 • Kula matunda yaliyoliwa nusu na wanyama wenye maambukizi.
Image result for marburg virusMAKUNDI YENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA MAAMBUKIZI
Kila mtu yupo kwenye hatari ya kuambukizwa.
Makundi yenye hatari Zaidi ni kama
Watu wote wanaoishi na au kuhudumia wagonjwa wa Marburg
Waombolezaji kwa kugusa mwili wa marehemu kama sehemu ya utaratibu wa mazishi
Wawindaji
Watoa huduma za afya.DALILI ZA UGONJWA WA MARBURG
Dalili huanza kujitokeza kati ya siku 2 hadi 21 baada ya kupata maambukizi

 • Homa kali ya ghafla
 • Maumivu ya kichwa
 • Maumivu ya mwili misuli na viungo
 • Kuharisha majimaji(kunakoweza kuambatana na damu)
 • Maumivu ya tumbo(abdominal pain and cramping)
 • Kutokwa na damu puani,mdomoni,machoni,masikioni,na sehemu ya haja ndogo na kubwa.
 • Kutapika.
 Image result for marburg virus symptoms


TIBA KWA MGONJWA WA MARBURG
Hakuna tiba ya ugonjwa huu wala chanjo.
Mgonjwa hutibiwa kwa kutegemea dalili:
Tiba ya homa na maumivu
Kuongezewa damu na maji mwilini
Tiba lishe

JINSI YA KUJIKINGA
Njia za kujikinga na ugonjwa huu ni pamoja na
Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono au kukumbatiana
Epuka kugusa damu,matapishi,mkojo,kinyesi,kamasi,mate,machozi na majimaji mengine yanayotoka mwilini mwa mtu mwenye dalili za ugonjwa huu.
Nawa mikono na maji yanayotiririka na sabuni mara unapomtembelea mgonjwa hospitalini au kumhudumia.
Wahi kituo cha kutolea huduma za afya unapoona dalili za ugonjwa wa Marburg

#NINI KINATAKIWA KUFANYIKA
Kutoa elimu kwa jamii juu ya ugonjwa huu na namna ya kujikinga na ugonjwa huu
Kuwajengea uwezo watumishi wa afya namna ya kuwahudumia wagonjwa wenye dalili za ugonjwa huu
Kuimarisha kamati za kukabiliana na maafa / majanga
Kuhakikisha kuwepo kwa dawa na vifaa tiba vya kutosha na vifaa vya kujikinga
Kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa kwa kutoa taarifa kama kuna mtu yeyote atakayeisiwa kuwa na ugonjwa huu.

ANGALIZO
NI muhimu kutoa taarifa mapema kutokana na kuwa ugonjwa huu hauna tiba halisi na huweza pelekea kifo kwa asilimia kubwa,hata hivyo matibabu yake ni kutibu dalili za ugonjwa.


IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
Post a Comment
Powered by Blogger.