MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTUMIA NJIA YA KALENDA KUPANGA UZAZI

Njia ya kutumia kalenda ya uzazi wa mpango ni mojawapo ya njia ambazo hukadiria ni wakati gani mwanamama huweza kupata ujauzito, na misingi yake ni uelewa na kuweka rekodi ya mizunguko ya hedhi ya miezi iliyopita.

Muhimu ya kuzingatia
Mwanamama anaweza kutumia Njia ya wanaopata siku za hedhi za kawaida kama siku zake za mzunguko wa hedhi ni kati ya siku 26 hadi 32 kwa urefu. Kama mwanamama atakuwa na mizunguko ya hedhi zaidi ya 2 ndani ya mwaka ambayo ni mirefu au mifupi ukilinganisha na mizunguko ya kawaida ya hedhi, njia hii ya kawaida ya kalenda haitaweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Vifaa vinavyohitajika
Kalenda, kalamu, simu ya mkononi (ukipenda)

Jedwali la maelekezo
Fuatilia na weka rekodi ya siku za mizunguko ya hedhi.
  •    Mwanamama afuatilie siku za mzunguko wake wa hedhi, akihesabu siku ya 1 pale anapoona siku zake.
Epuka tendo la ndoa bila kinga kati ya siku ya 10 hadi siku ya 20.
  •   Siku ya 10 hadi ya 20 ya mzunguko hedhi, mwanamama mwenye mzunguko wa kawaida anaweza kupata mimba.
  •   Wapenzi waepuke tendo la ndoa bila kutumia kinga.Waweza kutumia kinga kama kondomu kuanzia siku ya 10 hadi 20.
  •   Wapenzi wanaweza kufanya tendo la ndoa bila kinga siku ya 1 hadi ya 9, tangu mwanamama aanze kuona siku zake, pia anaweza kushiriki tendo la ndoa bila kinga kuanzia siku ya 20 hadi atakapoona siku zake za mzunguko unaofuata.

Tumia viweka kumbukumbu
  • Mwanamama anaweza kutumia kalenda kwa kuweka alama ili kuepuka kusahau. Katika zama hizi za sayansi na teknolojia pia simu yako ya mkononi yaweza kutumika kwa kutega milio ambayo itakukumbusha siku maalum.IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
Post a Comment
Powered by Blogger.