JE, NI KWELI MAFUTA YA TAA HUPUNGUZA HISIA ZA KIMAPENZI (LIBIDO)?

Watu wengi wamekuwa na mitazamo tofauti tofauti juu ya uhusiano kati ya mafuta ya taa (kerosene) na hali au hisia za kimapenzi (libido). Wapo wanaosema kuwa mafuta ya taa hupunguza hisia za kimapenzi, pia wengine wanaona hakuna uhusiano wowote wa vitu hivi viwili. Yawezekana hujawahi kukutana na kisa hiki, ila kwa walio wengi waliowahi kusoma shule za bweni (boarding schools) nadhani kitu hiki siyo kigeni kwaoJe ukweli ni upi?

Ukweli ni kwamba hakuna uthibitisho wowote kisayansi unaoonesha kwamba Mafuta ya taa yanapunguza hisia au hamu ya kufanya mapenzi(libido),hakuna ushahidi wowote wa kitaalamu unaoonesha kama mafuta ya taa yakiingia mwilini huleta mabadiliko yoyote katika hormones.

Mafuta ya taa hutumika kusaidia kuongeza utendaji kazi wa utumbo(bowel movements) hivo kusaidia watu wenye tatizo la kutopata choo kupata.

Lakini pia kitaalamu kula kiwango kikubwa cha mafuta ya taa pia ni sumu mwilini inaweza kupelekea utumbo kutofanya kazi vizuri( kuziba kwa utumbo)
Post a Comment
Powered by Blogger.