JE KIPIMO CHA MIMBA KINASOMA BAADA YA MUDA GANI?

Muda gani mzuri wa kupima mimba ni upi?
Unapotaka kubeba mimba au unapokua na wasiwasi kwamba umepata mimba, mara nyingi hua ni changamoto kwa wasichana kwani wengi wao hujikuta wanapima siku hiyohoyo au kesho yake kuangalia kama mimba imeingia kitu ambacho hata kwa vipimo vya kisasa zaidi huwezi kupata majibi sahihi kwa muda mfupi hivyo.
Muda mzuri wa kupima mimba kwa uhakika zaidi ni pale unapokosa siku zako za hatari za mwezi unaofuata, kipindi hiki zile homoni ambazo kitaalamu ndio zinasomwa kwenye mkojo mtu akiwa na mimba kwa jina la human chorionic gonadotrophin hormone zinakua tayari ziko za kutosha hata kwa vile vipimo ambavyo havina nguvu sana vinasoma kwa uhakika.

Muda unaotumika kwa kipimo kusoma inatofautiana kwa wanawake tofauti..
Wakati unataka kupima mimba unatakiwa ujue kwamba wanawake wanatofautiana sana wao kwa wao kutokana na urefu wa mizunguko yao yaani wengine mizunguko mirefu na wengine mfupi.
yai la mwanamke na mbegu ya mwanaume vinapokutana huchukua siku saba mpaka kumi kuweza kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi, baada ya hapo baada ya siku mbili mpaka tatu ndio mimba inaweza kusoma...
Hivyo kwa ujumla tunasema inaweza kuchukua siku 14 mpaka siku 21 kusoma kama mimba imeingia au haijaingia baada ya kulala na mwanaume. wanawake wengine hutokwa na damu kidogo mimba inapojishikisha kwenye ukuta wa uzazi kitaalamu tunaita implantation bleeding, damu hii hua inakua kidogo sana kuliko ile ya kawaida ya hedhi lakini kipindi hiki mimba inakua bado haijasoma kwenye kipimo.

Unatakiwa upime saa ngapi?
Kila unavyopima kipimo cha mkojo, unakua unapima homoni ya human chorionic gonadotrophin hormone ambayo nimeitaja hapo juu.
Muda mzuri ambayo homoni hiyo inaonekana ni asubuhi, hivyo zingatia kupima mimba asubuhi kwa majibu mazuri zaidi, wakati mwingine ukipima mchana unaweza kuona mistari ambayo inafifia yaani haina rangi nyekundu ya kutosha.
Post a Comment
Powered by Blogger.