UTAFITI: WATU WENGI HUWA VIZIWI KWA KUONDOA NTA YA SIKIO

watu wengi huona nta iliyopo sikioni kama uchafu hivyo hujijengea tabia ya 
kuiondoa mara kwa mara bila kujua kuwa huwa na kazi muhimu ndani ya sikio.
Mtaalamu huyo alisema kuwa, nta ina kazi nyingi. Kazi hizo ni kama vile kuzuia vijidudu vya magonjwa visiathiri sehemu ya ndani ya sikio, kuzuia vumbi, 
kulainisha ngozi ya ndani ya sikio na kuhusika katika kuchuja sauti sambamba na viungo vingine vilivyopo ndani ya sikio.
Kutokana na faida hizo, endapo mtu atakuwa na tabia ya kuiondoa nta kila mara, tena kwa kutumia vijiti vya pamba ‘pamba stick,’ huwa katika hatari ya kukosa faida zilizoainishwa hapo awali na kujisababishia madhara kama vile muwasho ndani ya sikio (itching) kutokana na bakteria wa fangasi na vumbi ambalo litakuwa likiingia bila kizuizi.
Hatari ya pili ni kukauka kwa ngozi ya ndani ya sikio na maumivu makali hasa kama mtu huyo atakuwa katika mazingira yenye kelele nyingi na mwisho kabisa ni kuharibika kwa ngoma ya sikio na mfumo mzima wa usikivu.
Hata hivyo, pamoja na faida hizo za nta ndani ya sikio ni vyema mtu akajua kwamba nta ikizidi sikioni huweza kusababisha kuziba kwa sikio, kusababisha kizunguzungu na kuhisi karaha (discomfort) hivyo ni vyema kama mtu atakuwa 
akiondoa nta hiyo angalau mara moja kwa kila miezi miwili kwa afya yake.
“Nta huwa uchafu kama itazidi sikioni ni vyema kujiwekea ratiba ya kuondoa kila baada ya miezi miwili kuliko kufanya hivyo kila mara,” alisema Dr. Bujiku.


IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
Post a Comment
Powered by Blogger.