MWILI WA AGNES GERALD "MASOGANGE" KUAGWA KESHO

Mwili wa aliyekuwa msanii wa video za muziki wa Tanzania, Agnes Gerald maarufu Masogange unatarajiwa kuagwa kesho katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea kwao Mbeya kwa ajili ya mazishi.

Dada wa Marehemu Flora amesema tayari familia imeshakaa na wasanii wenzake na kufikia makubaliano hayo.

Agnes amefariki jana majira ya saa kumi jioni katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Post a Comment
Powered by Blogger.