Mwenyekiti UVCCM Kasema Hamtambui Wema Sepetu, Kuzungumza Kung'olewa kwa Jokate

Mwenyekiti wa UVCCM Kheri James amefunguka na kuwazungumzia Jokate na Wema Sepetu katika umoja huo wa vijana wa CCM.

Akizungumza katika kipindi cha kikaangoni live kinachorushwa na EATV. mwenyekiti huyo amesema kuwa hawezi kuzungumzia swala lolote kuhusu kuondolewa kwa Jokate katika nafasi hiyo kwa sababu wakati wanamueweka hawakuzungumzia katika media.

“Kama ambavyo hatukuweza kuweka wazi kuhusu kuteuliwa kwake Jokate, ndivyo ambavyo hatuwezi kuzungumzia kutolewa kwake. Kuhusu Wema kwakweli Wema mimi simjui,namsoma tu kwenye magazeti kuwa amerudi CCM na sio UVCCM”-Kheri James


March 25 mwaka huu Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM ilitengua uteuzi wa aliyekuwa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa umoja huo, Jokate Mwegelo.


Pia utakumbuka February 24, 2017  Wema alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akitokea Chama cha Mapinduzi (CCM) December 01, 2017 alitangaza kurejea CCM.

Post a Comment
Powered by Blogger.