Kakobe ahojiwa Uhamiaji

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amesema yeye ni raia wa Tanzania ,"anayesema mimi si raia wa Tanzania aniambie ni raia wa nchi gani."
Askofu Kakobe ametoa kauli hii leo Aprili 9,2018 mara baada ya kutoka kuhojiwa kwa takriban saa tatu kuhusu uraia wake katika Ofisi ya Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema uhamiaji wanaweza kuwa na nia njema lakini, "kwa nini sasa, kwa nini wanahojiwa watu wa aina fulani wa kutoka eneo fulani la Kigoma. Mbona hatujasikia kutoka Dodoma, Kaskazini wakihojiwa."
"Mimi ni Mtanzania na kama kuna mtu anasema si raia basi aniambie mimi ni raia wa nchi gani," amesema Askofu Kakobe
Amesema, ametakiwa kuacha hati yake ya kusafiria ili iweze kuwasaidia kupata taarifa zake muhimu huku yeye akisisitiza "hiki wanachokifanya kina tia shaka.
Mahojiano ya kiongozi huyo wa kiroho yaliyoanza Saa 4.53 asubuhi hadi saa 7.55 mchana yamehitimishwa
Post a Comment
Powered by Blogger.