JE WATAKA KUJUA : HENRY 'BOX' BROWN MTUMWA ALIYEAMUA KUJISAFIRISHA KWENYE BOX KAMA MZIGO KWA LENGO LA KUKWEPA UTUMWA.

Henry 'Box' Brown: Mtumwa aliyeamua kujisafirisha kwenye box kama mzigo kwa lengo la kukwepa utumwa. 
March 23 Mwaka 1849 Henry Brown aliyekuwa mtumwa Kwenye Jimbo la Virginia akisaidiwa na rafiki yake mzungu alitengenezewa box maalum lililokuwa na matundu ya kuingiza hewa, Brown aliwekwa kwenye sanduku hilo kwa lengo la kusafirishwa kwenda Philadelphia kwa James Miller McKim ambaye ni mzungu anayepinga utumwa.

Safari ya kusafirisha box hilo ilitumia masaa 27 kupitia kwenye gari, boti na treni huku Brown akila biscuits na kunywa maji aliyowekewa kwenye box hilo. Uhai wa Brown ulikuwa shakani baada ya box hilo kuwekwa juu chini kwa muda wa dakika 90 Hali iliyopelekea Brown kusimamia Kichwa kwa muda wote Huo. Brown alifika salama na akawa huru. Brown alichukua maamuzi hayo baada ya kushuhudia mke wake na watoto wake wakiuzwa kama watumwa kwenye jimbo lingine

IMEANDALIWA NA MOSES MUTENTE
Post a Comment
Powered by Blogger.