Chanzo na suluhisho la ugumba kwa wanaume


CHANZO NA SULUHISHO LA UGUMBA KWA WANAUME
Watu wengi hudhani kama mwanamke hapati ujauzito basi tatizo na lawama zote zitakuwa ni upande wa mwanamke, lakini hilo si lazima mara zote liwe hivyo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa tatizo la kutopata mtoto katika familia likawa linatokana na ugumba upande wa mwanaume.
Visababishi vya ugumba kwa mwanaume:
Kuna sababu kuu 2 za ugumba kwa mwanaume, nazo ni mbegu chache na homoni kutokuwa sawa.

1. MBEGU CHACHE (low sperm count):
Ni moja ya kisababishi kikubwa cha ugumba kwa wanaume wengi. Ni mhimu wenza wote kufanya vipimo inapobainika wamekaa muda mrefu bila kupata mtoto. Wakati wanawake wanahitaji vipimo vingi kujua chanzo cha ugumba wao, wanaume wao wanahitaji kipimo kimoja tu nacho ni cha kujua uwingi wa mbegu na afya ya mbegu kwa ujumla (sperm analysis).
Vipo vipimo vidogo vya kawaida kwa ajili ya kupimia uwingi wa mbegu unavyoweza kuvitumia hata mwenyewe binafsi ukiwa nyumbani au unaweza kumuona daktari kwa vipimo vya jumla zaidi.
Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua milioni 20, chochote chini ya hapa kinaweza kuwa sababu ya kutokutungisha ujauzito.
Ikitokea umegundulika kuwa na mbegu chache, ni nyepesi sana na hazina nguvu za kukimbia vya kutosha basi makala hii itakupa maelezo juu ya dawa za asili zinazoweza kukusaidia hilo.
Visababishi vya mbegu kuwa chache
Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume, kwa bahati nzuri vingi ya vitu hivyo tunao uwezo wa kuvidhibiti kwa kupunguza matumizi yake.

Vitu hivyo ni pamoja na:
• Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume. Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta.
Unashauriwa kutokuweka simu ndani ya mfuko wako wa suruali kwa kipindi kirefu na kutokuweka kompyuta mpakato (laptop) kwenye mapaja yako wakati wote ukiitumia. Ni muhimu pia kutokutumia masaa mengi kutwa nzima ukiwa kwenye kompyuta.

• Vifaa vya Intaneti visivyotumia waya – Siku hizi tofauti na zamani, kuna teknolojia mpya imeingia ya kuunganisha intaneti kwa kutumia vifaa visivyotumia waya (wireless internet) au kwa lugha nyepesi hujulikana kama Wi-Fi.
Vifaa hivi vinapunguza wingi wa mbegu, uwezo wa mbegu kukimbia na kuharibu muundo asili wa mbegu kwa ujumla (DNA fragmentation). Wanaume wenye tatizo la uzazi wanashauriwa kutotumia aina hii ya vifaa vya kuunganishia intaneti kwenye kompyuta zao na vile vile kutokuweka simu kwenye mifuko yao ya mbele ya suruali.

• Uvutaji wa Sigara – Uvutaji sigara, bangi na bidhaa nyingine za tumbaku huharibu ubora wa mbegu za kiume. Hilo halihitaji majadiliano. Habari njema ni kuwa madhara yaliyosababishwa na uvutaji sigara yanaweza kurekebishika ikiwa tu utaamua kuacha kuvuta. Huhitaji dawa kuacha kuvuta sigara, unahitaji kuamua tu kwamba sasa basi na hakuna lisilowezekana kwa mtu mwenye maamuzi na mwenye ndoto za maisha mazuri ya kiafya.

• Viuavijasumu na homoni katika vyakula – Viuavijasumu (pesticides) vinavyotumika katika mazao mbalimbali mashambani miaka ya sasa ni sababu mojawapo ya tatizo la homoni kutokuwa sawa kwa wanaume wengi.
Kwenye bidhaa nyingi za maziwa za viwandani sasa huongezwa homoni kama vile homoni ya estrogeni ambazo hazihitajiki katika mwili wako. Vyote hivi vina madhara katika afya ya mwanaume.

• Vyakula vyenye soya – Vyakula vyenye soya ndani yake hasa vile vya viwandani kama vile maziwa ya soya, burger za soya nk si vizuri kwa afya ya uzazi ya mwanaume. Vinasemwa moja kwa moja kuathiri ubora wa homoni ya testosterone homoni mhimu sana kwa afya ya uzazi wa mwanaume

• Unywaji pombe – Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.

• Matumizi ya vifaa vya plastiki – Wakati kifaa cha plastiki kinapowekewa chakula cha moto hutoa kitu kijulikanacho kama ‘xenohormones’ ambacho huigiza kama ni ‘estrogen’ ndani ya mwili na hivyo kupelekea matatizo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume.

• Joto kupita kiasi (Hyperthermia) – Mifuko ya mbegu za uzazi ya mwanaume inahitaji joto la chini kidogo ya lile joto la mwili kwa ujumla ili mbegu zibaki na afya. Inasemekana kuwa hii ndiyo moja ya sababu viungo vya uzazi vya mwanaume vipo karibu nje kabisa ya mwili wake.
Joto linajulikana wazi kuharibu ubora wa mbegu na hivyo itakuwa vizuri kuepuka mazingira ambayo yanaweza kusabbaisha joto la moja kwa moja kwenye viungo vya uzazi vya mwanaume ikiwemo kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana.

• Mfadhaiko (Stress) – Mfadhaiko au stress inaweza kuleta majanga makubwa katika homoni na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.
Stress inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.
Vile vile kuna presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai. Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na tatizo la kupungua kwa mbegu na uzazi kwa ujumla.
Kuwa na amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, just relax kila kitu kina muda wake.

• Aina ya chakula unachokula – Chanzo kingine cha kuwa na mbegu chache au zisizokuwa na afya ni kutokula chakula sahihi na cha kutosha kila siku. Kwa afya bora kabisa ya uzazi mwanaume anahitaji vyakula vyenye madini ya zinki (zinc) kwa wingi, selenium, Vitamin E, folic acids, Vitamini B12, Vitamini C na vyakula mbalimbali vinavyoondoa sumu mwilini (antioxidants).

• Kujichua (punyeto) – Hili ni janga kubwa miongoni mwa wanaume wengi wengi karibu kote duniani. Tabia hii ukiianza huwa ni vigumu kuiacha na ni rahisi sana kugeuka kuwa teja wa punyeto. Madhara makubwa ya kujichua ni pamoja na kupungua kwa kasi kwa uwingi wa mbegu kwa mwanaume pia nguvu zake kwa ujumla na hivyo kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito.

2. USAWA WA HOMONI USIO SAWA (Hormone Imbalance):
Tatizo la homoni kutokuwa sawa si jambo linalowapata wanawake peke yao, ni jambo linalojitokeza pia kwa wanaume ingawa wengi wao huwa hawana muda wa kufikiri kuwa nalo. Homoni zina umhimu mkubwa katika kazi ya uzalishaji wa mbegu na katika afya ya uzazi wa mwanaume kwa ujumla.
Moja ya homoni kuu inayohusika na uzazi kwa mwanaume ni homoni ya testosterone. Kutokana na maisha yetu ya kisasa na baadhi ya matatizo yaliyoelezwa hapo juu upande wa uwingi wa mbegu, wanaume wengi wanajikuta katika hali hii ya kuwa na tatizo la homoni zao kutokuwa katika usawa unaohitajika kwa afya bora ya uzazi.
Vipo vitu vinavyoweza kuharibu homoni ya testerone na huanza kwa kuigiza au kijifanya vyenyewe ni estrogens (xenohormones). Estrogen ikizidi katika mwili wa mwanaume hupelekea uhanithi (uume kushindwa kusimama), kukosa hamu ya tendo la ndoa, kupungua kwa mbegu na kupungua kwa maji maji ya mbegu kwa ujumla.

Visababishi hasa vya kuharibika kwa testeroni ni pamoja na
• Vyakula vyenye soya
• Madawa yanayotumika katika mazao mashambani
• Homoni zinazoongezwa katika bidhaa za maziwa na nyama
• Vifaa au vyombo vya plastiki

Tafadhari usitumie dawa yoyote bila ruhusa au uangalizi wa karibu wa tabibu. Kufanya hivyo unaweza kujiongezea matatizo mengine zaidi bila mwenyewe kujua.


IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
Post a Comment
Powered by Blogger.