Ajali ya basi, Noah yaua wanane

Watu wanane wamekufa papo hapo baada ya basi la abiria kugongana na Toyota Noah.
Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Aprili 9, 2018 mchana eneo la Igodima nje kidogo ya Jiji la Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu amesema basi hilo lilikuwa likitokea jijini Mbeya kwenda Isangawanya wilayani Chunya.
Amesema Toyota Noah ilikuwa ikitokea mjini Chunya kuelekea Mbeya mjini.
Kaimu kamanda amesema waliofariki dunia walikuwa kwenye Toyota Noah iliyokuwa na watu tisa.
Post a Comment
Powered by Blogger.