ZIJUE SABABU NA MATIBABU YA DAMU YA HEDHI KUWA NA MABONGE

Mwanamke huingia kwenye hedhi kwa wastani wa muda wa siku 3 mpaka 7. Katika kipindi hiki hutoa damu kwa wastani wa mililita 30 – 80 kwa siku, damu ikiwa nyekundu bila mabonge yoyote. kiasi hiki cha damu ni sawa na kutumia pedi 2 mpaka 3 kwa siku bila kulowa damu chepechepe.
Kuna wakati mwanamke anaweza kupata damu yenye mabonge, yaani iliyoganda na nyeusi. Hali hii huashiria kiasi cha damu anachopoteza ni kingi zaidi ya kawaida. Inaweza kuambatana na hedhi kuwa ndefu zaidi ya kawaida au damu kutoka nyingi zaidi ya kawaida.
Hali zifuatazo zinaweza kusababisha hili;
 • Sindano za kuzuia mimba
 • Mimba kutoka
 • Vitanzi vya kuzuia mimba (Intrauterine Contraceptive Devices)
 • Endometrial hyperplasia
 • Maambukizi ya Via vya uzazi vya ndani (Pelvic Inflammatory Disease – PID)
 • Vivimbe kwenye ukuta wa mji wa uzazi (endometrial polyps)
 • Mabonge kwenye mji wa mimba (uterine fibroids)
 • Saratani ya ukuta wa mji wa uzazi, mji wa uzazi au shingo ya uzazi.
Matibabu

Unapopata hali hii ni vizuri uonane na daktari haraka iwezekanavyo. Uchunguzi na vipimo vikifanyika tatizo linaweza kujulikana na kutibika. Matibabu yanaweza kujumuisha;
 • Dawa za kupunguza maumivu
 • Vidonge vya homoni
 • Kitanzi chenye homoni
 • Kusafisha mji wa uzazi (Dilatation and Curretage)
Imeandaliwa na Doctor Joh Blog

Post a Comment
Powered by Blogger.