Wema Sepetu apata shavu Wasafi Tv

Staa wa Filamu Bongo na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu amesema kuwa, kipindi chake kipya ndani ya kituo cha runinga cha Wasafi (Wasafi Tv) kitakuwa msaada mkubwa kwa jamii, kwa kuwa kitagusa, na kuchambua matatizo yao moja kwa moja.
Wema anatarajia kuwa mmoja wa watangazaji wa vipindi vya kijamii ndani ya Wasafi Tv itakayozinduliwa hivi karibuni.
Akizungumzia hatua hiyo, Wema alisema anamshukuru Mungu kwa kupata nafasi hiyo ya kufanya kipindi ambacho ameeleza kitakuwa na msaada mkubwa sana katika maisha ya watu mbalimbali.
Alisema, amewahi kufanya vipindi kadhaa huko nyuma ambavyo vilikuwa na mashabiki wengi, lakini ndani ya Wasafi Tv atakuja na kipindi cha tofauti na alivyozoeleka.
Kituo hicho na Wasafi Radio vitakuwa chini ya mwanamuziki Diamond Platnumz ambaye huko nyuma amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanadada Wema Sepetu.
Post a Comment
Powered by Blogger.