Namna ya kuondoa wadudu kwenye nyumba yako

Ukiachilia matatizo kama panya, mbu ndani ya nyumba, lipo tatizo sugu la wadudu aina ya mende, ambao kwa baadhi ya nyumba ni kama wanafamilia.
Nasema kama wanafamilia kwa sababu ni sugu na wenye nyumba ni kama wameshindwa kuwamaliza na kubaki kulalamika ” Nyumba hii kwa kunguni!!”.
Kuna sababu nyingi zinazowafanya wadudu hao kuwa wengi ndani ya nyumba, ikiwamo uchafu unaotokana na mrundikano ama wa vitu au takataka kwenye kona, pembe, penyo za nyumba.
Wanakuwa wanafamilia zaidi iwapo usafi hufanyika kwa kubagua baadhi ya maeneo, kutoinua vitu kila siku wakati wa kufanya usafi hivyo, hivyo kuwapa nafasi ya kukaa na kuzaliana.
Kuna mambo kadhaa ambayo yakifanyika kwa umakini na lengo la kuwafukuza mende yanaweza kuleta mafanikio ikiwamo kupanga vitu kwa mpangilio unaostahili.
Mpangilio huo wa vitu haubagui iwe nguo, viatu, ndoo za maji, mifuniko na mifuko ya karatasi na plastiki isiyotumika au iliyokwishatumika lakini imerundikwa.
Jambo lingine la kuzingatia ili kukabiliana na mende pamoja na kufanya usafi wa uhakika, kuzingatia eneo la kutupa mabaki ya chakula liwe mbali na nyumbani.
Muhimu pia na kutumia dawa, sabuni wakati wa kufanya usafi, badala ya kutumia maji peekee. Itapendeza zaidi kama angalau mara tatu kwa wiki unafanyika usafi wa nguvu utakaouhusisha kutoa vyombo vidogo nje ili usafi ufanyike kila mahali.
Katika kukabiliana na mende usafi hivyo ni bora kupunguza vitu visivyokuwa na matumizi kama vile mifuniko ya ndoo, viatu visivyovaliwa, nguo, madaftari ya zamani na matambara ya deki yasiyotumika.
Post a Comment
Powered by Blogger.