Mwanafizikia maarufu Stephen Hawking Afariki Dunia

Mwanafizikia maarufu duniani Prof Stephen Hawking amefariki dunia akiwa na miaka 76, familia yake imetangaza.
Mwingereza huyo alifahamika sana kwa kazi yake ya kisayansi kuhusu uwepo wa eneo katika anga za juu ambapo nguvu za mvutano huwa za juu sana kiasi kwamba miali haing’arishi au hata mwanga hauwezi kuponyoka.
Kwa Kiingereza, eneo hilo hufahamika kama ‘Black Hole’, Alitumia hilo katika kujaribu kufafanua kuhusu asili ya vitu vyote duniani na angani.
Alikuwa mwandishi wa vitabu kadha maarufu vya sayansi kikiwemo A Brief History of Time (Historia Fupi kuhusu Wakati).
Watoto wake, Lucy, Robert na Tim, wamesema: “Tumehuzunishwa sana kwamba baba yetu mpendwa ametuacha.”
“Alikuwa mwanasayansi muhimu na mtu wa kipekee ambaye kazi zake na mchango wake vitaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi.”
Stephen Hawking alipokuwa na miaka 22 pekee aliambiwa na madaktari angeishi miaka mingine miwili pekee baada yake kupatikana na ugonjwa nadra sana wa mfumo wa neva.
Ugonjwa huo ulimfanya kulemaa na kulazimika kutumia kiti cha magurudumu.
Nyakati za mwisho za maisha yake, alikuwa hawezi kuzungumza ila kwa kutumia kifaa cha kufasiri mawazo yake na kuyageuza kuwa sauti.
Post a Comment
Powered by Blogger.