Moto wakatisha uhai wa familia ya watu wanne

Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuteketea moto.
Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Magwira, Kata ya Bwilingu wilayani Chalinze usiku wa kuamkia leo Machi 11, 2018.
Chanzo cha moto hakijajulikana ingawa imeelezwa kulikuwa na tatizo la umeme kuzima na kuwaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shanna amethibitisha tukio hilo akiahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.
Post a Comment
Powered by Blogger.