NJIA MBILI ZA KUYAFANYA MENO YAKO KUWA MEUPE NA YA KUNG’AA

Kinywa ni moja kati ya vitu vinavyopaswa kufanyiwa usafi wa kina katika mwili, ili kujikinga na madhara mbali mbali ikiwemo harufu mbaya ya mdomo.
Katika kusafisha kinywa, meno hutakiwa kusafishwa siyo tu kwa sababu ya kuyafanya yang’ae na kuonekana meupe, bali pia kuyalinda dhidi ya bakteria wabaya wanaoweza kuyaharibu meno yako na kupelekea kuyang’oa.
Leo tutaona jinsi ya kusafisha meno kwani wengine wana ya rangi ya njano kutokana na vyakula pamoja na vinywaji tunavyokunywa. Pia inategemea ni vipi unatunza afya yako ya meno, kama unapiga mswaki vizuri, unasafisha vizuri.
Kama meno yako si ya rangi ile inayotakiwa, chagua kati ya hizi njia mbili za kutumia mara moja kila wiki. soma hapa njia mbili za kusafisha meno yako ili yawe meupe.

Baking Soda na Juisi ya ndimu
Baking soda ina sodium bicarbonate ambayo inasaidia kuondoa madoa na rangi ukichanganya na ile juisi ya ndimu inasaidia kupunguza alkaline iliyopo kwenye ndimu.

Changanya juisi ya ndimu pamoja na baking soda kupata mchanganyiko mzito, futa meno kuondoa mate kisha chukua mswaki wako, chota mchanganyiko kisha paka kwenye meno (usipige nayo mswaki kama unavyotumia dawa ya mswaki, paka tu), iache kwa dakika moja kisha sukutua na maji. Fanya hivi mara moja kwa wiki.

Tumia mafuta ya nazi
Tumia mafuta ya nazi kila asubuhi kusukutua kabla hujapiga mswaki. Weka kiasi cha kutosha mdomoni kisha anza kusukutua, zungusha katika kila kona, fanya kama unavuta na kuyasukuma humo mdomoni lakini usiyameze. Fanya hivi kwa dakika 10-15. Ukishamaliza hivyo sukutua kisha piga mswaki kama kawaida, dawa hizi zina uwezo wa kulinda meno na wadudu na kuyatakatisha.
Post a Comment
Powered by Blogger.