NASSARI ASHTAKIWA KWA SHAMBULIO

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru kujibu shtaka la shambulio.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Fortunatus Muhalila mbele ya hakimu Jasmine Abdul amedai Desemba 14, 2014.
Nassari alimshambulia Neeman Ngudu. Anadaiwa kutenda kosa hilo eneo la Makiba kwa kumpiga mateke Ngudu na kumsababishia maumivu akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Muhalila amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na ameiomba Mahakama kupanga siku nyingine ya kutajwa shtaka hilo.
Nassari anayetetewa na wakili Sheki Mfinanga alikana kutenda kosa hilo. Hakimu Abdul aliahirisha kesi hadi Machi 6,2018 itakapotajwa. Nassari alidhaminiwa na diwani Gabriel Mwanda wa Kata ya Ambuseri aliyesaini bondi ya Sh5 milioni.

Chanzo:  Mwananchi

Post a Comment
Powered by Blogger.