Mambo ya msingi anayopaswa kuyajua mtu anayejifunza kuendesha gari

Kumiliki gari ni jambo la muhimu kwa watu wengi kwa sababu tunahitaji gari kwa ajili ya kazi, familia au kufanya mizunguko ya hapa na pale ya kuwatembelea ndugu, jamaa na marafiki.
Kumiliki gari kunakwenda sambamba na kufahamu jinsi ya kuendesha gari, lakini ukiwa unamiliki gari unatakiwa kujua mambo kadhaa muhimu yanayohusiana na kuendesha chombo hicho.
Kufahamu kuendesha gari ni jambo ambalo linapitia hatua mbalimbali. Hatua hizi zinahusisha mafunzo maalumu ambayo yatamwezesha mtu kufahamu kwa undani jinsi gani ya kutumia gari.

Vifuatavyo ni vitu ambavuo mtu anayejifunza kuendesha gari anatakiwa kuvitambua ili iwe rahisi kwake kurndesha gari hilo.

Rejeta (Radiator)
Kazi ya chombo hiki ni kuhifadhi kimiminika cha kupoozea injini (coolant). Chombo hichi ni muhimu kwa sababu huhifadhi kimiminika hicho kinachotumika kupooza injini ya gari lako wakati wote inapokuwa imewaka ili isipate joto kubwa ambalo linaeza kupelekea madhara mengine mengi katika gari lako.

Kilainmishi (Oil)
Kazi ya oil ni kulainisha vyuma vilivyoko katika gari, sana sana kwenye injini ili visisagane na kuharibika. Oil hupunguza kasi ya msuguano wa vyuma na upungufu au ukosefu wa oil katika injini ya gari lako kunaweza kupelekea injini yako kufa au kusimama (knock).

Mafuta ya breki (Brake Fluid)
Kazi ya mafuta ya breki ni kusaidia gari kupunguza mwendo au kusimama kabisa pale unapokanyaga breki. Mafuta haya yakipungua, yanaweza kusababisha gari lako kukosa breki au kutumia umbali mrefu kusimama tofauti na awali (kutokuwa na breki nzuri), jambo ambalo linahatarisha usalama wako, gari lako, magari mengine na watumiaji wengine wa barabara. unashauriwa kukagua mara kwa mara kiwango cha mafuta hayo kama yamepungua na ubaini chanz kilichoasababisha mafuta hayo kupungua, huenda kuna sehemu ya ‘pipe’ imepasuka na inahitaji kuzibwa.

Betri (Battery)
Kazi ya betri ni kuhifadhi chaji ambayo hutumika katika kuwasha gari, kuwasha vitu kama vile taa na redio katika gari lako. Betri ya gari lako inapokuwa haifanyi kazi vizuri unaweza ukashindwa kuwasha gari lako (start engine), na vitu vingine vinavyohitaji kutumia umeme katika gari lako.

Ignition Coil
Kazi ya ignition coil ni kukuza moto utokao kwenye betri na kuingia kwenye distributor ambayo nayo nayo hutoa umeme kwenye plugs ukiwa umepoa.

Distributor
Hii hugawanya umeme kwenye injini na kufanya gari kuwa na mlio mzuri na nguvu. Chombo hiki kina nyaya tano na ukichomoa waya mmoja tu, gari linakuwa na tatizo la ku-miss.

Plugs.
Hutumika kusaidia kuchoma mafuta ya petroli au diesel kwenye injini. Plug zinaposhindwa kufanya kazi inabidi ubadilishe kwani gari lako halitowaka na pia likiwaka litakuwa lina ‘misfire’.

Fuel Pump
Hutumika kuvuta mafuta kutoka kwenye tenki na kuyasukuma kwenye Carburetor.

Carburetor
Hii nayo hupokea mafuta kutoka kwenye fuel pump na kuyachanganya na hewa kwa kipimo maalumu kilichowekwa kisha kuyaingiza kwenye injini.

Altenator
Chombo hiki ndicho kinachofua umeme wakati wote gari linapokuwa limewaka. Ndiyo maana unaweza ukajiuliza niwapi betri yako inapopata chaji wakati hujawahi kuitoa na kuichaji, kifa hiki ndicho huichaji betri ya gari lako wakati wote. Kifaa hiki kinaposhindwa kufanya kazi, basi betri ya gari yako itakuwa inatoa tu umeme pasipo kupata umeme wa kuichaji, hivyo mwisho wa siku itaishiwa chaji na kushindwa kuendelea kufanya kazi.

Self-start
Kazi ya self start ni kuwasha gari pale linaposhindwa kujiwasha lenyewe (likiwa bovu). chombo hichi hufanya kazi wakatu gari linaposukumwa na kushtuliwa.

Gear box
hili ni box ambalo lina mkusanyiko wa gia zote za gari lako kuanzia ndogo mpaka kubwa. Unapoendesha gari na kubadilisha gia, basi shughuli yote ya upangiliaji wa gia kulingana na ulivyochagua wewe hufanyika ndani ya chombo hichi.

Differential
Hugawanya mwendo unaotoka kwenye injini na kuupeleka kwenye matairi.
Post a Comment
Powered by Blogger.