HATUA TANO ZA KURUDISHA NGUVU ZA KIUME KATIKA NDOA YAKO

Nguvu za kiume hapo zamani za kale na tafiti za kisayansi zinaonesha ni matokeo yanayotokea uzeeni kuwa ni jambo la kawaida kwa umri mkubwa, lakini napenda nikwambie kuwa uzeeni ambao unaambatana na magonjwa sugu kiasi hicho ni moja wapo ya sababu nikuweke kwenye kundi la watu wanaozeeka vibaya. Kwa kawaida binadamu hustahili kuzeeka na magonjwa tunazeeka na magonjwa kwa sababu tunayasababisha sisi
kwa maisha ya kifahari tunayoishi na kusahau kuwa afya yako sio hazina ya milele,unatakiwa kuiheshimu,kuilinda na kuimarisha ili uje ufurahie uzee wako usio na magonjwa.

Najua kuwa hadi sasa ukifanya tafiti vijana wa umri wa miaka 20 hadi 30 ndio wanao ongoza kwa kusumbuka na matatizo haya ya nguvu za kiume tofauti na matarajio yetu wote kuwa tatizo hili tunasoma kuwa linawapata wazee, swali la kujiuliza kwa nini sasa vijana tena katika umri mdogo? Ndio maana nimeamua kukuandikia Makala hii ambapo kama ni miongoni mwa watu wanaosumbuka hili tatizo nina uhakika tatizo lako utapata suluhisho kutokana na elimu hii rafiki yangu. Pia najua unaweza ukawa na mchumba wako, unavumulia mengi kuhusu tatizo hili la mwenzi wako, usiwe mkimya kwani inahitaji utashi wa juu sana kumweleza mwenzi wako kuhusu hili swala kwani upungufu wa nguvu za kiume unasababisha msongo wa mawazo wengine hupelekea hadi kuchanganyikiwa hatimaye kupata MAJOR DEPRESSIVE DISORDER na mbali na hivyo husababisha kutokujiamini na woga wa kuwa na mke na hivyo wengi wamejaa wasiwasi na hofu kubwa ya kugunduliwa na mwezi wake kuwa ana tatizo hilo, na wengi wao ni woga sana kutogunduliwa tatizo hilo,ndio maana inapofikia hatua mwenza wako umembaini ni mara chache sana atakubali kuwa kweli ana tatizo hilo. Kwa nini usumbuke na matatizo kama haya wakati msaada wako upo? Usiendelee kusumbuka na tatizo hili kwani umeumbiwa maisha ya furaha na Mungu ni haki yako kufurahia uumbaji wa Mungu, anza leo kushughurikia tatizo kabla halijawa sugu mpendwa msomaji wa Makala hii.


NINI KISABABISHI MSINGI WA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME?
Katika mwili wa binadamu kuna vichocheo aina ya Testosterone ambavyo hutolewa malengo ya kuimarisha utendaji kazi wa ubongo,ufanye kazi katika hali tulivu,kuondoa,kuondoa msongo,kuondoa mstuko wa aina yoyote ,kuimarisha uwezo wa kufikiri,kuimarisha furaha ya mwili wako na hatimaye kuimarisha nguvu za kiume na hatimaye kufurahia tendo la ndoa. Kazi kubwa ya kichecheo hiki ni kuhakikisha mwili wako unakuwa katika hali tulivu kabisa kwa kuutuliza ubongo wako ndipo utafurahia ndoa yako rafiki yangu.
Sasa endapo kichecheo hiki kikivurugika kinasababisha vichocheo vingine kama insulin,leptin,cortisol,vichocheo vya ukuaji pia kuvurugika kwani matokeo ya hitililafu hii mwilini inasababisha  KUPUNGUKIWA NGUVU ZA KIUME kwa sababu vichocheo hivi vinafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa, na endapo kimoja tu kikivurugika vyote vinapoteza mwelekeo na tatizo kuwa sugu Zaidi.
Napenda leo nieleze kwa kina kidogo namna gani nguvu za kiume zinapotea kutokana na mvurugiko wa vichocheo hivyo vikuu vitatu kama nilivyo vitaja hapo juu.

1.       TESTOSTERONE
Kichocheo hiki ndio silaha ya mwanaume kwani ndicho kichocheo ambacho kinakufanya uwe na sifa zote za kiume na ndicho kicheo ambacho kinakufanya uwe imara katika tendo la ndoa. Upungufu wa kicheo hiki kinasababisha kupungua kwa matamanio kwa jinsia tofauti,kupungua kwa nguvu za misuli yako kiutendaji,mafuta kurundikana ovyo mwilini( BELLY FAT AND OBESITY)
Lakini pia ijulikane kuwa kichocheo hiki cha testosterone sio kwamba kinapatikana kwa wanaume tu, la hasha! Kichocheo hiki hata wanawake wanacho ingawaje kwa kiwango cha chini sana, endapo kinapokuwa kimepungua kinaweza kumsababishia mwanamke kukosa matamanio kwa jinsia ya kiume wakati wa tendo la ndoa, kukosa nguvu ya misuli ya kuhimili tendo la ndoa (Kuchoka Sana),kuongezeka uzito kupita kiasi na nyama uzembe pia kupunguza uwezo wako katika kufikiri na kumbu kumbu.

NINI KINASHUSHA TESTOSTERONE MWILINI MWAKO?
Moja ya kisababishi kikubwa cha testosterone kushuka kiwango chake ni kwa sababu ya kuwepo na kizuizi cha insulin (insulin resistance) hii inafanya kiwango cha insulin kuwa juu sana na kusababisha testosterone kushuka kiwango chake. Moja ya sababu zinazo sababisha kiwango cha insulini kuwa juu sana ni unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda na pia ulaji wa vyakula vyenye vionjo mbalimbali vitamu vilivyotengenezwa viwandani. Hivyo basi sukari inapokuwa ipo katika kiwango cha juu sana kwenye damu inasababisha utolewaji wa insulin kuwa katika kiwango cha juu pia kwenda kusawazisha sukari irudi kawaida. Hivyo basi matumizi ya vyakula na vinywaji vya sukari nyingi vinafanya mwili upate kizuizi katika utendaji kazi wa insulin na hatimaye testosterone pia kushuka kiwango chake. Najua umejifunza sasa kwa nini watu wanaotumia vyakula vya viwandani,vinywaji vya sukari nyingi,ulaji wa vyakula vyenye mafuta mabaya jinsi gani inasababisha vichocheo vyako kushuka kiwango na unaendelea kusumbuka sana. Napenda kukuambiwa kuwa siku zote watu hawaogopi vyakula vyenye sukari wanaogopa vyakula vyenye mafuta mengi, hio ni fikra potofu sana! Sugar is more addictive than heroin and cocaine, kwa maana nyingine watu ni walevi wa vyakula na vinywaji vya sukari na haipo siku anaweza kuacha haraka. Usihofu kama una tatizo hilo ujue tayari umeshaathiriwa na ulaji wa vyakula na vinywaji hivyo.

2.       INSULINI
Hiki ni kichecheo ambacho hutolewa na kongosho lako ili kwenda kusawazisha kiwango cha sukari mwilini mwako. Kazi kubwa wa maji haya ya insulin ni kuhifadhi nishati ya mwili kwa matumizi ya baadae pale mwili unapokuwa una nishati ya kutosha na hautaki kupoteza nishati ya ziada. Nishati hii huhifadhiwa asilimia kubwa  katika mfumo wa glycojeni mwilini mwako kwenye misuli,ini nk. Sasa inapotokea kiwango chako cha ulaji wa vyakula vya sukari ni kikubwa sana ndivyo kiwango kingi cha insulin kitatengenezwa na kumwagwa kwenye mzunguko wa damu kwenye kuhifadhi sukari ya ziada ambayo haitumiki wakati ule na hatimaye kusazisha kiwango cha sukari mwilini mwako. Kazi ya insulin sio kushusha sukari kama wengi tunavyofundishwa darasani! Kwa nini nasema hivi? Kazi ya insulin ni kuhifadhi nishati ya ziada kwa matumizi ya baadae na hivyo basi kupungua kwa sukari ni matokeo ya kazi ya insulin mwilini mwako.

HEBU SOMA TAFAKURI HII:
Umeingia katika chumba ambacho umekuta harufu mbaya sana ya deodorant spray au perfume punde tu utakapo ingia katika chumba hicho utasumbuka sana na harufu hio kwa muda mfupi na hatimaye unaizoea na kuona ni harufu ambayo haina madhara wala usumbufu kwako.
Huu mfano utakusaidia kujua kwa nini tunasema insulin yako imeshindwa kufanya kazi, na umepata kizuizi katika utendaji kazi wake. Nimesema insulin hutolewa kwa kiwango kikubwa sana kulingana na kiwango cha sukari mwilini mwako, kiwango hiki kingi cha insulin kwenye damu kwa muda mrefu inaweza kupelekea insulin kupoteza kazi yake kiuhalisia. Na pia kitu kingine ambacho kinaweza kupelekea insulin kutofanya kazi ni vipokea insulin kutoitikia kwa sababu ya mafuta mabaya kuleta kizuizi katika vipokezi vya insulin. Vitendo vyote hivi viwili vinasababisha kiwango cha insulin kuwa juu wakati wote  na kama nilivyo eleza mwanzo kuwa kiwango cha insulin kinavyozidi kuwa kingi mwilini mwako kinashusha vichocheo vya Testosterone ambavyo ndio silaha yako mwanaume. Hivyo basi ukiangalia katika maelezo haya utagundua kuwa ulaji wa vyakula na vinywaji vingi vya sukari vinasababisha kiwango cha insulin kuwa juu muda wote ambapo nacho kinapelekea vichocheo vya kiume kushuka na hatimaye unakumbwa na matatizo ya kukosa matamanio kwa jinsia tofauti,msongo wa mawazo,misuli kukosa nguvu muda wote umechoka,uzito kuongezeka kwa kasi sanana wengine hupelekea kumilki vitambi.
Pia kiwango kingi cha insulin kwa muda mrefu kwenye damu kinaweza kupelekea kupata nywele usoni kwa wanawake,mwanaume kuishiwa vinyweleo sehemu kama kifuani,tumboni na maeneo mengine mengi.

3.       LEPTINI
Hiki ni kichocheo cha pekee sana na huwa napenda sana kukizungumzia kwani kinaonesha jinsi gani binadamu alivyo umbwa kwa kutumia teknolojia ya uhandisi wa hali ya juu. Hiki ni kichecheo ambacho kinatengenezwa na seli zinazohifadhi mafuta ambazo zinapatikana kwa wingi kwenye misuli kazi yake kubwa ni kupeleka ujumbe kwenye ubongo katika kuendesha hamu yako unapokuwa una chakula mbele yako, na ubongo huitikia kwa kutoa taarifa ya kutosheka na chakula kwa kujihsi umeshiba na huwezi tena kuendelea na chakula.
Sasa basi ulaji wa vyakula vingi bila mpango vyenye sukari nyingi unasababisha seli za kuhifadhi mafuta (FAT CELLS) kutengeneza kwa wingi leptin ili kwenda kutimiza kazi yake. Kiwango cha insulin na leptin hupanda kwa pamoja kama mapacha vile. Hivyo hivyo kumbuka tafakuri ile pale juu ya perfume, itafikia wakati kiwango kingi sana kinasababisha leptin kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi yake ( KUKATA HAMU YA CHAKULA) hivyo utakuwa una tatizo la kula mlo mkubwa ambao hata siku moja hautosheki na ukitosheka muda si mrefu unahitaji tena kula. Hawa ndio watu wengi ni wahanga wa muda wote wanapenda kula vyakula vitamu vitamu tu, hamu haiishi (Sugary addicted,sugar craving) na wengi huishia kupata matitizo ya kiafya kama kuishiwa nguvu za kiume,uzito kupita kiasi,kitambi na kuishiwa nguvu kabisa ya misuli yote haya ni kwa sababu kiwango kingi cha leptin na insulin kinashusha vicheo vyako vya testosterone.

4.       CORTISOL
Hiki ni kichocheo ambacho hutolewa na mwili pale unapokuwa katika hali yoyote ya mstuko ili kwenda kukabiliana na mtuko huo.
Mfano labda Dr Boaz Mkumbo nilikuwa natembea njiani ghafla nikaona nyoka huyo mkubwa chatu. Mwili utastuka sana na kutoa vichecheo vinavyo enda kupambana na hio hali iliyoshtua mwili wako, mfano cortisol huenda kuongeza kiwango cha nishati ya mwili (glucose) kwenye damu na kuwa na nguvu ajabu ya kumkimbia adui yako aliyepo ,mbele yako.
Cortisol pia hutolewa hata kama mwili wako umekabiliwa na mstuko ndani kwa ndani mfano,sukari mwilini imepungua mwili unatoa cortisol ambayo kazi yake kubwa ni kubadili ile nishati iliyokuwa imehifadhiwa katika mfumo wa glycogen kwenye misuli na ini kuwa sukari na hatimaye kuongeza sukari mwilini mwako.
Sasa tafiti zinasema kwamba,kiwango kingi cha cortisol kwenye damu kinachosababishwa na msongo,mstuko ndani ya miili yetu inayo endelea inasababisha LEPTIN kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi yake ipasavyo.
Na endapo leptin ikishindwa kufanya kazi yake ipasavyo utakuwa una tatizo la kula sana hasa vyakula na vinywaji  vya sukari bila hamu kukata na hatimaye kusababisha insulin kupanda juu na testosterone kushuka chini na hatimaye kuishiwa nguvu za kiume,matamanio kwa jinsia tofauti nk.
Hongera sana kwa kuendelea kusoma Makala hii, hapo juu nilitaka kukueleza tu nini kinatokea endapo unapatwa na upungufu wa nguvu za kiume kwani wengi mmekuwa mkinipigia simu kutaka kujua kwa nini nguvu za kiume sasa, basi leo nazani umejifunza kitu, kama hujaungana nami katika ukurasa wangu facebook hebu bofya like Dr Boaz Mkumbo MD utafurahia Makala zangu nyingi sana nzuri zimeandaliwa kwa ajili yako.
Basi napenda nikupe vitu vikuu 4 vinavyo angamiza watu kukosa nguvu za kiume hawa ndio maadui wako wakuu kuhusu tatizo lako hilo mpendwa, hebu endelea kusoma upate suluhisho lako,ufurahie ndoa yako,

VITU 4 VINAVYO ANGAMIZA NGUVU ZAKO ZA KIUME NA KUKUACHA MWENYE MSONGO WA MAWAZO NA MPWEKE KATIKA MAHUSIANO AU NDOA YAKO
Hebu basi napenda nikwambie hawa maadui wako, najua utashangaa kuwa ni maadui ambao kila siku ni marafiki zako, na hujui kuwa wanaangamiza msingi wa ndoa yako na inaweza kuwa unajua lakini unayapuuzia haya tunayokufundisha kupitia elimu hii ya afya, huwa napenda kuwaambia wagonjwa wangu kuwa afya yako ni mali yako sio ya daktari wala muuguzi wewe ndiye una mamlaka ya afya yako kuiweka sawa au kuidhoofisha.  Hivyo napenda kukuambia kuwa afya yako sio hazina ya milele linda sana afya kuliko vyovyote ulindavyo kwani ndio msingi wa furaha zote duniani.
Post a Comment
Powered by Blogger.