Updates: Rais Magufuli amfuta kazi Kamishna wa Madini Mhandisi Mchwampaka

Aliyekuwa Kamishna wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamini Mchwampaka 

Rais Magufuli amemfuta kazi Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na kumteua Prof Shukrani Manya kuchukua nafasi hiyo. Rais amefanya uteuzi huo akimuapisha Naibu Waziri wa Madini, Mbunge Doto Biteko. Mhandisi Mchwampaka amedumu katika nafasi hiyo kwa siku 263.

"Nimeambiwa Kamishna wa Madini ni tatizo, inawezekana yupo hapa. Nimeamua kumteua Profesa Shukrani Elisha Manya, atakuwa Kamishna wa Madini, na ndiye atakuwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini." - Rais Magufuli
Post a Comment
Powered by Blogger.