Ujue ugonjwa wa kisukari: Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Ugonjwa wa Kisukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu. Sukari hutumiwa na mwili ili kupata nishati lishe. Ili mwili uweze kutumia sukari inayotokana na vyakula, unahitaji kichocheo cha insulin. Insulin husaidia sukari kuingia kwenye chembechembe hai ili kutengeneza nishati lishe. 

Ugonjwa wa kisukari unasababishwa na kichocheo hiki kupungua au kutofanya kazi kama inavyotakiwa, hivyo kiwango cha kisukari kinabaki kikubwa kwenye damu kwa sababu sukari haikuwezeshwa kuingia kwenye chembechembe hai za mwili.

Tafiti za ugonjwa wa kisukari zinaonyesha kuwa mwaka 2007 kulikuwa na wagonjwa 246 milioni duniani. Takwimu za mwaka 2012 zinaonyesha kuwa kulikuwa na wagonjwa 371 milioni ulimwenguni kote, Takwimu za mwaka 2013, zinaonyesha kuwa kulikuwa na wagonjwa 382 duniani kote.Ifikapo mwaka 2035 kutakuwa na wagonjwa 592 millioni. Katika bara la Afrika kulikuwa na wagonjwa wa kisukari 19.8 millioni mwaka 2013 na wataongezeka mpaka million 41.4 ifikapo mwaka 2035, ambapo nusu ya wagonjwa hawa walikuwa hawajaanza matibabu. Asilimia 80 ya wagonjwa wote wa kisukari ulimwenguni wanaishi katika nchi zinazoendelea, ikiwemo Tanzania.
Utafiti uliofanyika mwaka 2012 na kuhusisha wilaya 50 nchini Tanzania ulionyesha ya kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wana ugonjwa wa kisukari. Katika nchi 10 zinazoongoza kwa kisukari Barani Afrika Tanzania inashika nafasi ya 8.

Dalili za Kisukari
Mara nyingi, watu wengi hawajitambui ya kuwa wana ugonjwa huu. Wengine wanakuwa na dalili lakini hawachukui hatua mapema. Dalili za kisukari ni rahisi kuzitambua nazo ni: kiu isiyoisha, kukojoa mara kwa mara, kupungua uzito, kusikia njaa kila wakati na mwili kukosa nguvu. Ukiwa na dalili hizi nenda hospitali ukapime sukari.


Mgonjwa pia anaweza kuona dalili ya kuchoka haraka, kupungua uzito, vipele mwilini ambavyo kitaalamu huitwa diabetic dermadromes.

Mgonjwa wa kisukari pia huwa katika hatari ya kupata maambukizi katika kibofu cha mkojo, ngozi na kwa wanawake sehemu za siri. Aidha kuna dalili maalumu ambazo hutokea kwa wagonjwa wa kisukari iwapo mgonjwa atapatwa na mojawapo ya madhara (complications) ya ugonjwa huo.

Madhara hayo ambayo hujulikana kwa kifupi DKA hutokea kwenye aina ya kwanza ya kisukari na huwa na dalili zifuatazo: Mgonjwa kutoa harufu ya acetone inayofanana kidogo na harufu ya pombe.
Mgonjwa pia hupumua kwa haraka na kwa nguvu, kujihisi kichefuchefu, kutapika, kuhisi maumivu ya tumbo na kupoteza fahamu. Kupoteza fahamu mgonjwa kunakoitwa Hyperosmolar Non-ketotic coma hutokea kwenye kisukari cha aina ya pili ambapo mara nyingi husababishwa na upungufu wa maji mwilini.


Tiba ya ugonjwa wa kisukari
Kwa Bahati mbaya ugonjwa wa Kisukari hauna tiba kamili hivyo pale unapokupata utaendelea kuwa nao lakini ugonjwa wa kisukari unaweza kudhibitiwa na malazi mazuri, virutubisho, mazoezi na tiba mbadala ya ugonjwa wa kisukari inayotakiwa kuifanya kabla ya tatizo halijawa kubwa.


Kwa hali ya kawaida wataalamu wa afya hupendekeza lishe ambayo si tiba ya ugonjwa wa kisukari lakini unaweza kurudisha virutubisho muhimu ambayo vinaweza kukosekana kutokana na ugonjwa wa kisukari.

Bidhaa za afya za Optimum Diabetics – 80 pointi. Kisukari optimum zimekuwa zikiandaliwa na kutumika kutoa msaada wa lishe kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari.

Kila kuongezeka kwa kinga ni lazima kukamilisha, full-potency ya uundaji wa vitamini, madini sanifu na Extracts ya mitishamba hasa kwa mara zote kula chakula bora kitokanacho na optimum Diabetics Afya Supplement ambayo hutoa virutubisho vinavyokosekana mwilini na kama ikitumika vizuri kwa miezi sita tatizo la Kisukari hupungua kabisa namara nyingine Kuisha kwani lishe hii inasaidia kwa asilimia 80%.
Post a Comment
Powered by Blogger.