UJUE UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA NYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA - CHANZO, DALILI NA TIBA

Tatizo  la  kutoka  na  kinyama  ama  uvimbe  katika  sehemu  ya  haja  kubwa  hujulikana  kama  Bawasiri.

Katika  lugha  ya  kitaalamu  ugonjwa  huu  hujulikana  kama haemorrhoids  ilihali  katika  lugha  ya  kiingereza, hujulikana  kama  Piles.


Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe
Tatizo hili huwaathiri zaidi watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu asilimia 50 ya idadi ya watu wote wako hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 50.


Ingawa dalili zake zinaweza zisijitokeze, lakini tatizo hili huwa na madhara kama kuvuja damu, kuporochoka kupitia tundu la haja na maumivu.Aina Za Bawasiri :
Kuna aina mbili za bawasiri

- Bawasiri ya nje:Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. 

Mara nyingine, mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina ya bawasiri ambayo kitaalam inaitwa Thrombosed hemorrhoid.


-Bawasiri ya ndani:
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa  na   huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.

Hutokana na kuvimba na kuharibika kwa vimishipa vya aina ya artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa.


Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:

Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
- Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je, bawasiri husababishwa na nini?Chanzo chake kikuu kitaalam hakijulikani, ingawa mambo yafuatayo yanaweza kusababisha au kukuweka katika hatari ya kupata bawasiri:
i.                    Tatizo sugu la kuharisha
ii.                   Kupata kinyesi kigumu
iii.               Ujauzito
iv.                uzito kupita kiasi (obesity)
v.                  Mazoezi ya kunyanyua vitu vizito
vi.                Kuingiliwa  kinyume  na  maumbile
vii.              Umri mkubwa
viii.           Mambo yanayoongeza shinikizo katika utumbo  mpana kama kukaa muda mrefu mahali pamoja
ix.               Matumizi ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu kuliko vya kuchuchumaa na kujisaidia kwa mda mrefu wakati wa haja.

    Dalili za bawasiri
i.                    Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia
ii.                  Maumivu au usumbufu wakati wa kujisaidia
iii.                Kinyesi kuvuja
iv.                kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
v.                   Ngozi  kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
vi.                Na kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa.


Matatizo yanayoweza kutokana na bawasiri:
- Kupata upungufu wa damu (anemia)

- Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo
- Kupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
- Kuathirika kisaikolojia

Vipimo na uchunguzi:

Kipimo cha kidole cha shahada kwa njia ya  puru (Digital Rectal Examination), Kipimo cha njia ya haja kubwa cha kutazama moja kwa moja (Proctoscope) na Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)


Matibabu yakeMatibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri, pia tiba mara nyingi si ya upasuaji, mfano mgonjwa ataelekezwa kukalisha eneo la haja kubwa katika maji ya vuguvugu kwa mda fulani, ipo tiba rahisi iitwayo Rubber band ligation
Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, njia hii hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.

Tiba Ya Asili Ya Bawasiri :Unaweza  kujaribu  mwenyewe  mojawapo kati  ya tiba  zifuatazo.  Kila  tiba  inajitegemea  hivyo  unashauriwa  kuanza  na  tiba  moja  kwanza na  uangalie  matokeo  yake kabla  ya  kuhamia  na  tiba  nyingine,usitumie  tiba  zote  kwa  wakati  mmoja.

- Hakikisha unapata choo la laini wakati hivyo unaweza kufanya yafuatayo.
- Kunywa maji mengi
- Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi mfano matunda mboga za majani na vyakula vya nafaka.
- Epuka dawa za maumivu zenye codaine mfano
- Nenda chooni mara tu unapohisi haja.Usijaribu kubana.
Post a Comment
Powered by Blogger.