Wem Sepetu arudi CCM

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ametangaza kurudi CCM baada ya kukaa Chadema kwa muda wa miezi kumi tangu alipohamia.
Katika ukurasa wake wa Instagram, Wema ameandika hivi, “Siwezi kuendelea kuishi kwenye nyumba inayonikosesha amani... Peace of mind is everything for me...natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi nyumbani.”
Mwigizaji wa filamu ambaye pia ni kada wa CCM, Steve Nyerere alipoulizwa kuhusu msanii mwenzake huyo kurudi CCM alisema ni kweli amefanya hivyo.
Akizungumza na waandishi akiwa ameambatana na mama yake mzazi nyumbani kwao Sinza Jijini Dar es Salaam wakati akihamia Chadema, Wema alisema sababu kubwa ya kuhamia ni ili kupata nafasi ya kupigania demokrasia anayodai kuwa inapotea nchini Tanzania.
Sababu nyingine aliyoieleza Wema ni kutelekezwa na CCM licha ya kujitolea kutoa mchango wake kwa chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kiasi cha kuwa hatarini kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar.
Hata hivyo, leo alibadili msimamo wake na kurudi CCM. Akizungumzia kuhama kwa Wema, Meya wa Ubungo, Boniface Jacob ambaye alipokea kadi ya CCM kutoka kwa Wema, alisema walikuwa bado hawajamkabizi msanii huyo kadi ya Chadema na kuwa walikuwa wanatafuta siku maalum ya kufanya hivyo.


Chanzo: Mwananchi
Post a Comment
Powered by Blogger.