WANAJESHI WAULA KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI LA ZIMBABWE


Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa ametaja bazara lake la mawaziri na kuwateua wanajeshi waandamizi katika nafasi za juu za uongozi.

Rais Mnangagwa amemteuwa Jenerali Sibusiso Moyo ambaye ndiye aliyezungumza kwenye television ya taifa kuhusiana na jeshi kutwaa udhibiti wa nchi hiyo kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Katika baraza hilo la mawaziri Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Anga, Perence Shiri, ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na Ardhi.
Post a Comment
Powered by Blogger.