WALIMU WALEZI WA SHULE ZA SEKONDARI WAPATIWA MBINU ZA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA, NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI.

 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai  akieleza namna Serikali inavyoshirikiana na wadau na wananchi kupambana  na Ukatili wa kijinsia katika siku ya mwisho ya mafunzo ya kuwajengea ulewa walimu walezi wa shule za Sekondari Tanzania katika kupambana ukatili hususan ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni kwenye mafunzo yaliyofanyika mkoani Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Familia Bi. Rose Minja akieleza jinsi Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisa,Wazee na Watoto ilivyojipanga kutokomeza Ukatili wa kijinsia katika siku ya mwisho ya mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu walezi wa shule za Sekondari nchini hususan kuzuia ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni kwenye mafunzo yaliyofanyika mkoani Dodoma.
 Mwakilishi wa Benki ya NMB PLC Bw. Rodgers Malangu  akieleza jinsia Benki hiyo inavyowezesha wazazi kuwekeza kwa watoto kwa lengo la kuwapa malezi na kuwafundisha utamaduni wa kuweka akiba kwa manufaa ya matunzo ya watoto wa Taifa hili katika siku ya mwisho ya mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu walezi wa shule za Sekondari Tanzania kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni yaliyofanyika mkoani Dodoma.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai akimkabidhi Cheti cha kuhitimu Mafunzo ya kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni kwa Mwalimu Mlezi wa Sekondari ya Sekondari Mnelo iliyopo mkoani Lindi Bw.Adam Matibwa katika siku ya mwisho ya mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu walezi wa shule za Sekondari Tanzania kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni yaliyofanyika mkoani Dodoma.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai akimkabidhi Cheti cha kuhitimu Mafunzo ya kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni kwa Mwalimu Mlezi wa Sekondari ya Sekondari Chang’ombe iliyopo Jijini Dar es Salaam Bw.Adam Matibwa katika siku ya mwisho ya mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu walezi wa shule za Sekondari Tanzania kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni yaliyofanyika mkoani Dodoma.
 Baadhi ya Walimu walezi kutoka mikoa 21 ya Tanzania Bara wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika siku ya mwisho ya mafunzo ya kuwajengea uwezo kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni yaliyofanyika mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai akiwa katika picha ya pamoja na walimu walezi wa shule za sekondari mara baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni yaliyofanyika mkoani Dodoma.

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Serikali kwa kushirikiana na wadau inaendeleza juhudi za kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni kwa kuwawezesha walimu wa shule za sekondari kwa kuwapa mbinu za kupambana na vitendo hivyo  katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai alipokuwa akifunga mafunzo ya kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni yaliyoandaliwa na walimu wenyewe kwa kushirikiana na Serikali na shirika la Femina.

Bi Magreth Mussai amesema kuwa katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia Serikali ilizindua Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Jinsia wa mwaka 2017/2018 hadi  mwaka 2020/2021.

Ameongeza kuwa katika kutekeleza Mpango mkakati wa Kupambana na ukatili wa kijinsia Wizara ilianzisha  kampeni ya kutokomeza ndoa na mimba za utotoni iliyozinduliwa na Wizara hivi karibuni Mkoani Mara inayosema: “Mimi ni Msichana Najitambua na Elimu ndio Mpango Mzima” 

Kwa upande wake Meneja wa Uhamishaji wa Femina Bi. Nashivai Molleli  amesema kuwa elimu walioyoitoa kwa walimu walezi hao itawasaidia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa weledi na uadilifu kama walezi wa wanafunzi shuleni katika kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni kwa kutoa elimu kwa wanafunzi, walimu, kamati za shule na jamii kwa ujumla.

Naye Mwalimu Mlezi wa  Shule ya Sekondari Mnelo ya mkoani Lindi Bw. Adam Matimbwa amesema kuwa  wao kama walimu walezi katika shule elimu walioipata ni muhimu sana kwao katika kuwapatia uelewa, maarifa, mbinu, na stadi za kumlinda mtoto wa kike, kuamsha ari ya wavulana kuwalinda wasichana wanaosoma nao, na kuwa mabalozi wa kushauri na kutoa elimu kwa makundi mengine wengine hasa wakiwemo walimu na vijana wa mitaani kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni katika maeneo yao ya kazi. Jitihada hizi zinalenga kupunguza na kutokomeza aina hizo za uaktili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/2022. 
Post a Comment
Powered by Blogger.