RC Simiyu akanusha kukamatwa na Takukuru

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Athony Mtaka amekanusha taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa amekamatwa na Takukuru.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa Mtaka amekamatwa na Takukuru kwa kugawa fedha za UVCCM kwenye uchaguzi.
Kutokana na taarifa hizo Mtaka amesema, “Kuna taarifa zinasambazwa kwamba nimekamatwa na Takukuru nikigawa fedha za UVCCM ni uzushi na uongo wa kupuuzwa.”

Chanzo: Mwananchi
Post a Comment
Powered by Blogger.