RC Kilimanjaro Anna Mghwira ahamia CCM

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amejiunga na CCM baada ya kueleza kuridhishwa nayo.
Akizungumza katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake CCM(UWT) baada ya Rais John Magufuli kumkaribisha Mghwira amesema ameona si vibaya kujiunga na CCM.
“Kutokana na kazi niliyofanya na serikali kwa kipindi cha miezi sita, nimependa kwa utaratibu mnaofanya katika utaratibu wa vikao,” amesema Mghwira.
Amesema anaiona CCM inayobadilika katika mkoa anaouongoza kwa kukataa rushwa. “Sioni kama kuna mtu anayetaka kubaki.”
Post a Comment
Powered by Blogger.