OFISI NZIMA YA MKIKITA WAHAMIA SHAMBANI VIKINDU KUPANDA MCHAICHAI

Mkurugenzi wa Fedha, Elizabeth akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui wakibeba miche ya mchaichai wakipeleka kupanda shambani Vikindu. Shmba hilo ni la wanachama wa Mkikita. 

Na Richard Mwaikenda
OFISI nzima ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen), umehamia shamba Vikindu kuanza kampeni ya kupanda mchaichai.

Katika kampeni hiyo ya aina yake iliwashirikisha wakurugenzi, maofisa na wafanyakazi wa mtandao huo ili kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Back to The Land.

Walipofika Block Farming hiyo ya mchaichai, waligawanyika katika makundi mbalimbali ambapo wengine kazi yao ilikuwa kubeba mbegu ya mchaichai, baadhi walisombelea mbolea, kufyeka majani, kuchanganya mbolea kwenye mashimo na wengine kupanda.

Kazi hiyo ilipamba moto hasa baada ya kuhamasishwa na viongozi wakuu ambao pia walishiriki bega kwa bega kubeba mbolea, mbegu na kupanda pia. Hakuna aliyeruhusiwa kukaa bila kazi akiwemo pia mwandishi wa habari hizi, Richard Mwaikenda.

Viongozi walioshiriki kwenye kampeni hiyo ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,  Dk. Kissui S. Kissui, Mkurugenzi Mtendaji,  Adam Ngamange, Mkurugenzi wa Utawala na Mashamba, Catherina, Mkurugenzi wa Fedha, Elizabeth na Mhasibu Mkuu wa mtandao huo, Mshashu na msaidizi wake Samson.

Ofisi kwa siku nzima ilibidi zifungwe kwa siku nzima, ambapo walifanya kazi ya shamba kwa siku nzima ya jana hadi majira ya saa jioni saa 12.
Meneja Uhusiano wa Mkikita, Neema (kulia0 akiwa na Ofisa wa Mradi wa Kuku, Rose wakati wa shughuli ya kupanda mchaichai
Adam akibeba mbolea kupeleka shambani
Dk. Kissui akiwa amebeba miche akipeleka shambani
Eva akifanya usafi kwenye shamba tayari kupanda mchaichai
Wakichambua miche ya mchaichai
Kazi ikiendelea
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mkikita, Dk Kissui (kulia) akiwapongeza wafanyakazi kwa moyo wao wao wa kujitolea kupanda mchaichai.
Post a Comment
Powered by Blogger.