NAZARETI YAFUTA MAADHIMISHO YA KRISMASI

Na Kituo cha Habari cha Palestina (Tanzania)
 Meya wa jiji la Nazareti  Ali Salam ametangaza kufuta maadhimisho  yaliyopangwa  kufanyika katika jiji hilo yenye mnasaba wa  Mwaka Mpya,isipokuwa sherehe za uwashaji wa mti wa krismasi na maandamano husika ya kimila ya kila mwaka. Uamuzi huo wa Mheshimiwa Salam, unalenga kupinga tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump kuitambua Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli.
Salam alisema hayo leo Alhamisi wakati wa mkutano wake waandishi wa habari kwamba: "Ndugu zetu Wapendwa katika jiji hili la Nazareti  lililo la thamani na kituo chetu cha Kiarabu kwa ujumla,  Kwa muda mrefu tulisema tunapokea maadhimisho ya Krismasi mara hii,yakiwa yanakwenda sambamba na taarifa za rais wa Marekani juu ya Jerusalemu na kuiunganisha kama mji mkuu wa milele wa Israeli,pamoja na nia yake ya kuhamishia ubalozi.
Tumeingia msimu wa maadhimisho kwa matarajio makubwa, ya kwamba uamuzi huu wa marekani ni wa dhulma, umeliingiza eneo zima katika kuchanganyikiwa na kutuondolea furaha ya sherehe na shamrashamra zake. Nilikuwa katika taarifa za manispaa za awali, nimethibitisha kuwa tupo pamoja na nduguzetu katika kila hali, tutafurahi wakifurahi na tutaona maumivu wakipatwa na maumivu.
Jerusalemu ilikuwa na itabaki kuwa taifa pendwa takatifu la kiarabu, likiwa ni mji mkuu wa Palestina na dora ambayo ipo katika taji. Aidha ameongeza kusema kuwa,"Shughuli za manispaa zitakuwa ni  kibiashara na kiuchumi tu kwa kulinufaisha jiji kibiashara, ambayo tulizoea kukusudiwa na idadi kubwa ya wageni katika msimu huu, huku kukiachwa kuthamini ufanyaji wa shamra shamra kwa taasisi za kidini na kijamii kwa uhuru kabisa, unaokwenda sambamba na mtazamo wao hali iliyopo.Post a Comment
Powered by Blogger.