MWANAMKE ACHOMWA MOTO NA MPENZI WAKE KWA KUKATAA KUCHUMBIWA NAYE

Mwanamke mmoja ajulikanaye kama Sandhya Rani mwenye umri wa miaka 25 huko Kusini mwa nchini India ameuawa kwa kuchomwa moto na mpenzi wake baada ya kukataa kuchumbiwa naye.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi katika jimbo hilo, mashuhuda wa tukio hilo wanasema waliona mwanaume huyo akifuata mwanamke huyo na wakaanza kuzungumza kwa kubishana na ndipo mwanaume huyo alipochukua mafuta ya taa aliyokuwa ametembea nayo na kummwagia binti huyo kisha kumuwasha moto.

Inaelezwa kuwa watu walijaribu kumwokoa binti huyo lakini alikuwa ameungua sana na alifariki akiwa njiani akipelekwa hospitali. 

Inaelezwa pia kuwa wawili hao wamewahi kufanya kazi ofisi moja. Polisi jimboni humo tayari wamemkamata mwanaume huyo aliyetambulishwa kwa jina la Karthika Vanga.
Post a Comment
Powered by Blogger.