Babu Seya, Papii Kocha waingia mtaani rasmi

Mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wametoka katika gereza la Ukonga jioni hii baada ya kusota kwa miaka 13.
Wanamuziki hao ‘baba na mwana’ walitoka katika kifungo cha maisha baada ya kupata msamaha wa Rais John Magufuli leo Jumamosi Desemba 9, mwaka 2017.
Rais John Magufuli  alitoa msamaha kwa baadhi ya wafungwa alipokuwa akihutubia Taifa kusherehea miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miongoni mwa waliopata ahueni hiyo ni Babu Seya na Papii Kocha.
“Babu, babu, babu,” zilikuwa ni kelele za mashabiki na ndugu zake waliompokea Babu Seya na Papii Kocha waliokuwa wametoka gerezani wakiwa na magitaa yao mgongoni.
Babu Seya aliyeonekana mtanashati alionekana anapunga mkono wa kulia kama mtu asiyeamini huku Papii Kocha akipunga mkono akionekana kufurahia na kuzungumza na mashabiki.
Walisindikizwa na askari magereza mpaka nje na kulikuwa na foleni kubwa kutokana na tukio hilo.
Post a Comment
Powered by Blogger.