ZANU-PF KUANZA MCHAKATO WA KUMVUA MADARAKA RAIS MUGABE

Chama cha rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye yupo matatani kwa sasa kimeanza mchakato wa kumchukulia hatua.

Afisa mmoja wa Zanu-PF amesema hoja ya kumvua madaraka ya urais Mugabe itawasilishwa bungeni hii leo, na mchakato huo utachukua siku mbili tu.

Hoja hiyo inamtumuhu Mugabe 93 makosa kadhaa likiwemo la kumruhusu mkewe Grace kujitwalia madaraka ya Kikatiba.

Viongozi wa kijeshi waliodhibiti nchi hiyo wiki iliyopita wamesema hivi karibuni watakutana na aliyekuwa makamu wa rais aliyekimbia uhamishoni baada ya kutimuliwa.
Post a Comment
Powered by Blogger.