WALIOFUATWA NA RELI KULIPWA FIDIA

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema nyumba zote zilizojengwa ndani ya hifadhi ya reli zitaendela kubomolewa bila ya kulipwa fidia yoyote.
Hayo amesema hayo leo mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Rodha Edward.
Mbunge huyo alitaka kufahamu kwamba Serikali inawasaidiaje wananchi wanaokumbwa na bomoa bomoa kupata fidia zao kwa wakati.
Amesema wananchi wengi wanaokumbwa na adha hiyo ni maskini na hawawezi kumudu gharama za ujenzi wa makazi upya.
Nditiye amesema katika kukamilisha ujenzi wa reli ya kimataifa asilimia 75 ya reli hiyo itapita katika hifadhi ya reli ya iliyopo sasa ilyojengwa kuanzia mwaka 1904.
“Wananchi wote waliopo ndani ya hifadhi ya reli hiyo wanatakiwa kuondolewa bila fidia kwa sababu walivamia eneo ambalo lilikuwa limetengwa lakini kwa wale ambao reli itawafuata wa utaratibu wa tathmini ya fidia unaendelea,” amesema Nditiye.
Na kuongeza kuwa "zoezi hilo linalenga kuwaondoa wavamizi wa eneo ambalo lilikuwa limetengwa tangu ujenzi wa kwanza," amesema
Amesema katika serikali ya awamu ya tano reli yenye urefu wa kilomita 4886 inatarajiwa kujengwa katika maeneo ya ukanda wa kati na kusini.

Chanzo: Mwananchi
Post a Comment
Powered by Blogger.