Wakili na Mkurugenzi TIB wapandishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

Washitakiwa ambao ni wakili maarufu wa kujitegemea Dkt. Ringo Tenga na Mkurugenzi mtendaji wa zamani wa benki ya rasilimali TIB Dkt. Peter Noni wamepandishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka sita likiwemo la utakatishaji wa fedha na kusababisha hasara ya dola milioni tatu na laki saba. 

Upande wa mashtaka ukiwakilishwa na wakili kutoka mamlaka ya Mawasiliano TCRA umedai washtakiwa wameingilia Mawasiliano na kusababisha hasara hiyo kupita simu za kimataifa kwa vipindi tofauti.
Post a Comment
Powered by Blogger.