UPDATES: MWIGIZAJI WA FILAMU LULU ATUPWA JELA MIAKA MIWILI

Mwigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amehukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia.
Hukumu hiyo imetolewa muda mfupi uliopita leo Jumatatu katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kuua bila kukusudia msanii mwenzake Steven Kanumba.
Watu mbalimbali wamejitokeza kufuatilia huku hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Maelezo ya Jaji Rumanyika: Ushahidi umejikita kwenye ushahidi wa mazingira hata mtuhumiwa alikubali.
"Mtuhumiwa alikubali marehemu alikuwa mpenzi wake na alikuwa naye siku ya tukio,"
"Walevi wanapolewa mambo mojawapo yanayoweza kutokea ni pamoja na kuanguka,"
"Mshtakiwa alijichanganya kama marehemu alikuwa kalewa hakusema kama wakati anamkimbiza aliwahi kuanguka."
"Wakati tunaambiwa kuwa daktari Parpas ni daktari wa familia hatukuwahi kuelezwa kuwa Josephine Mshumbusi kuwa ni daktari wa familia,"
"Mshtakiwa huyu akiwa ni mtu wa mwisho na marehemu ni nini hasa kilitokea. Mshtakiwa kipindi kile alikuwa mtoto wa miaka 16 ina maana alikuwa hajui jema na baya, lakini alikuwa ana uwezo wa kuitwa mke na kujua wapi pakwenda na muda gani wa kurudi."
"Kama mtoto ana uwezo wa kufanya mambo ya kiutu uzima akafanikiwa basi tutegemee iko siku Mahakama hii atafanya mambo ya kitoto na kuombwa alindwe."
"Sheria yakuua bila kukusudia inaleta udhibiti kuwa watu wanatakiwa wafanye mambo kwa tahadhari, wivu wa maendeleo huleta maendeleo wivu wa mapenzi huleta maangamizi."

Chanzo: Mwananchi
Post a Comment
Powered by Blogger.