POLISI YAMWACHIA 'BILIONEA' NYUMBA ZA LUGUMI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefikia uamuzi wa kumuachia Dk Louis Shika ‘bilionea wa nyumba za Lugumi’ baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kujidhamini yeye mwenyewe baada ya kukosa mtu yeyote aliyejitokeza kwenda kutaka kumwekea dhamana.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Novemba 14, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema “uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyefika kutaka kumwekea dhamana, yaani anaishi kama mtu wa nyikani.”
Mambosasa ameongeza, “nimeagiza watendaji wangu wamwachie kwa dhamana yaani ajidhamini yeye mwenyewe na awe anakuja kuripoti,” amesema Mambosasa
Kamanda huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya Mwananchi kumtafuta kutaka kujua hatima ya Dk Shika ambaye ameshikiliwa tangu Novemba 9 akituhumiwa kuvuruga mnada wa nyumba za kifahari za mfanyabishara Said Lugumi
Dk Shika tangu siku hiyo amekuwa gumzo sehemu mbalimbali kutokana na kile alichokifanya siku ya mnada alipokuwa akipandisha bei dhidi ya washindani wake na moja ya kauli zake zinaendelea kutumika hadi sasa ni ‘Mia 900 itapendeza.’

Chanzo: Mwananchi
Post a Comment
Powered by Blogger.