PICHA: MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMTEMBELEA LISSU HOSPITALINI NCHINI KENYA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika hospitalini hapo kumjulia hali leo tarehe 28 Novemba, 2017 jijini Nairobi nchini Kenya.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana walipofika hospitalini hapo kumjulia hali.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika hospitalini hapo kumjulia hali.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Msafara wa Samia umefika hospitalini hapa saa 11.43 jioni akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana.
Mwananchi lililokuwapo hospitalini hapo wakati Mama Samia, Balozi Chana na maofisa wengine wakiwasili hospitalini hapo.
Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.
Makamu wa Rais amefika hospitalini akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.
Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa Septemba 7.
Post a Comment
Powered by Blogger.