MTOTO WA MIAKA MIWILI AFANYIWA KITENDO CHA UKATILI CHA UBAKAJI NA KUTELEKEZWA PORINI HANDENI

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka miwili na miezi mitano amelazwa hospitali ya wilaya Handeni baada ya kufanyiwa kitendo cha ukatili cha ubakaji na kutelekezwa porini na aliyemfanyia kitendo hicho.
Akiongea kwa uchungu mama mzazi wa mtoto huyo amesema kuwa wakati wanatoka shamba yeye na mumewe wakasikia sauti ya mtoto kutoka msitu wa jirani na nyumbani kwao na wakahisi kuwa ni sauti ya mtoto wao na ndipo wakafuatilia na kumkuta mtoto analia kwa uchungu.

Nae mganga wa zamu wa hospitali ya wilaya Handeni amesema kuwa baada ya kumpokea mtoto huyo walimfanyia uchunguzi na kubaini kuwa amebakwa hali iliyomsababishia michubuko huku baadhi ya wananchi walio ongea na ITV wakitaka mhusika apewe adhabu kali.

Nae kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Benedict Michael Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa tayari mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi.


Chanzo: ITV Tanzania
Post a Comment
Powered by Blogger.