Madiwani wa CHADEMA watoka nje ya ukumbi

Baadhi ya madiwani wa Chadema katika halmashauri ya Manispaa ya Ilala wamesusia Kikao cha Baraza Madiwani kinachoendelea kwenye ukumbi wa mikutano Ilala jijini Dar es Salaam.
Madiwani hao wamefikia uamuzi huo baada ya Mkurugenzi kushindwa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa katika kikao kilichopita.
Kwa takribani dakika 50 madiwani hao walikuwa kwenye mvutano wengine wakitaka kikao hicho kiahirishwe hadi pale taarifa hiyo itakapowasilishwa.
Wengine walitaka kikao kiendelee kwa kupitia ajenda nyingine na taarifa hiyo ingefanyiwa kazi kikao kijacho.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Msongela Palela ameomba radhi kwa kushindwa kuwasilisha taarifa hiyo na kutaka busara zitumike kwa kuruhusu kikao kiendelee.
Baada ya mvutano wa muda mrefu hatimaye Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Naibu Meya wa Ilala, Omar Kumbilamoto ameamuru kikao hicho kiendelee ndipo baadhi ya madiwani hao wa Chadema walipoamua kutoka nje.
Hata hivyo Kumbilamoto ameeendeleza kikao hicho kikiwa na wajumbe pungufu.

Chanzo: Mwananchi
Post a Comment
Powered by Blogger.