ZAIDI YA WATU 20 WAUAWA KWA WAPIGWA RISASI LAS VEGAS MAREKANI

 Zaidi ya watu 20 wameuawa na takriban 100 kujeruhiwa kwenye ufyatuaji wAa risasi wakati wa tamasha huku Las Vegas. Marekani.

Mtu mwenye bunduki aliafyatua risasi kutoka ghoroga ya 32 kwenye hoteli ya Mandalay Bay, kwenda kwa tamasha lililokuwa likiendelea nje.
 Polisi wanasema mshukiwa ambaye alitajwa kuwa makaazi wa mji huo na ambaye hakutajwa jina ameuawa.
 Mamia ya watu walikimbia eneo hilo na milio ya risasi ikasikika kwa muda kwenye video zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii.
 Ufyatuaji huo ulitokea mwendo wa saa 05:30 GMT na walioshuhudia walisema kuwa mamia ya risasi zilifyatuliwa.
 Usafiri wa ndege ulisitishwa kutoka uwanja wa ndege wa McCarran mjini Las Vegas

  


Chanzo: BBC Swahili
Post a Comment
Powered by Blogger.