Mwigamba ajivua uanachama wa ACT-Wazalendo, ahamia CCM

Aliyekuwa kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba na baadhi ya wanachama wa ACT wametangaza rasmi kujivua uanachama wa ACT-Wazalendo na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari, Mwigamba amesema amefikia uamuzi huo baada ya viongozi wa ACT-Wazalendo kuwa na maamuzi ambayo ni tofauti na lengo la kuanzishwa kwa chama akitolea mfano kuipinga serikali hata katika shughuli za maendeleo.
“Uongozi wa sasa wa chama hiki unachepuka kwa kasi kubwa mno nje ya misingi ya chama na sasa chama kimebaki kuwa jahazi ambalo tanga lake limechanika na kukosa mwelekeo na hivyo kubaki kuyumbishwa kila upande kutegemea na mawimbi ya bahari ambayo yanalipiga jahazi hilo,
“Tumelazimika kutafakari na kuchanganua vyama vilivyopo vya siasa na baada ya tafakari yetu tumeamua kujiunga na CCM kwa sababu … CCM ya sasa ndiyo chamachama kinachoakisi kwa karibu itikadi, falsafa na sera za ACT-Wazalendo ambazo mimi na wenzangu tulishiriki kuziasisi,” alisema Mwigamba.
Mwigamba alisema wakati wanaanzisha chama cha ACT walikuwa na lengo la kuimarisha uzalendo, upendo, umoja na mshikanao kwa Watanzania bila kujali jinsia, dini au ufuasi wa chama cha siasa jambo ambalo ndilo CCM inasimamia.

“Tumjiridhisha mpangilio wa sasa wa CCM na serikali yake inatekeleza misingi hii kwa ustadi mkubwa mno tumeamua kujiunga na CCM ili tuendelee kuwa sehemu ya mapambano,” alisema Mwigamba.

Post a Comment
Powered by Blogger.