MADUKA 15 YA PEMBEJEO ZA KILIMO NA MIFUGO GEITA YAMEFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA

Maduka 15 ya pembejeo za kilimo na mifugo yaliyopo katika mji mdogo wa Katoro, Buseresere, Ushirombo na wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, yamefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wamiliki wake kukamatwa wakiuza aina 16 za viuatilifu kutoka nchi jirani ya Uganda ambavyo bado havijasajiliwa nchini na Taasisi ya udhibtiti wa viuatilifu kwa nchi za kitropiki ( TPRI ), kinyume cha sheria ya visumbufu vya mimea na mifugo ya mwaka 1997.
Operesheni hiyo ya kuyafungia maduka yanayouza viuatilifu feki na ambavyo havina usajili imeongozwa na mkaguzi mwandamizi wa TPRI Emmanuel Mausa ikiwa na lengo la kuhakiki viuatilifu wanavyouziwa wakulima na kubaini uelewa wa wauzaji wa viuatilifu iwapo wanaweza kutoa elimu sahihi ya matumizi sahihi ya viuatilifu kwa wakulima ili kulinda afya zao na mazingira kwa ujumla.

Mkaguzi huyo Mwandamizi wa TPRI, Emmanuel Mausa anaelezea changamoto wanazokumbana nazo katika udhibiti wa uingizaji wa viuatilifu ambavyo havijasajiliwa na kuthibitishwa na taasisi hiyo hasa katika maeneo ya mipakani na wito kwa wauzaji wa maduka ya viuatilifu.

Baadhi ya wakulima wa kijiji cha Buseresere wilayani Chato ambao wamezungumzia operesheni hiyo wamewashauri wakulima wenzao  katika maeneo mengine nchini kuepuka kununua viuatilifu feki na ambavyo havijasajiliwa kwa madai vinashusha tija ya kilimo, huku baadhi ya wauzaji wa viautilifu wakiipongeza TPRI kuendesha msako huo ili kulinda ubora wa bidhaa hiyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.