Wapinzani wasusia kuapishwa wabunge wapya CUF

Kambi ya Upinzani Bungeni imesusia kuapishwa kwa wabunge saba wa Viti Maalumu kutoka Chama cha CUF.
Wabunge hao wameapishwa leo Septemba 5 na Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Wakati wabunge hao wakitoka ndani ya ukumbi wa Bunge, waliobaki kushuhudia ni wabunge wa CUF, Magdalena Sakaya (Kaliua), Maftah Nachuma (Mtwara Mjini) na Maulid Mtulia (Kinondoni).
Awali, wafuasi wa CUF walifika asubuhi katika viwanja vya Bunge kushuhudia kuapishwa kwa wabunge hao walioteuliwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
Wafuasi hao waliambatana na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Habib Mnyaa walifika wakiwa kwenye magari matatu aina ya Toyota Coaster na mengine madogo yaliyokuwa yamebandikwa picha za Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Wabunge wa Viti Maalumu waliapishwa leo ni Alfredina Kaigi, Kiza Mayeye, Nuru Bafadhili, Rukia Kassim, Shamsia Mtamba, Sonia Magogo na Zainab Amir.
Hindu Mwenda, ambaye angeapishwa leo alifariki dunia Ijumaa Septemba Mosi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuzikwa Jumapili Septemba 3.
Post a Comment
Powered by Blogger.