VIDEO: DIAMOND PLATNUMZ AKIRI KUZAA NA HAMISA, AMUOMBA RADHI ZARI

Mwanamuziki Diamond Platnumz leo katika mahojiano yake na kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm, amekiri kuwa mtoto wa Hamisa ni wake.
Asema hakuna mazingira yoyote aliyotengeneza kumkataa mtoto kama inavyozushwa na alikuwa akitoa pesa kiasi cha Shilingi Laki 5 kila wiki kwa ajili ya matumizi. wanamuziki Diamond Platnumz amesema jina alilotoa apewe mtoto wake kwa Hamisa Mobetto ni Dylan lakini kwa sababu za kutafuta umaarufu mwanamke huyo alimwita Abdul Nassib.
Amesema Hamisa alimwita mtoto huyo Abdul ambalo ni jina la baba yake mzazi ili iwe rahisi watu kufahamu kuwa mtoto huyo ni wa kwake baada ya kukubaliana kufanya uhusiano wao kuwa wa siri.
“Mimi jina ninalolitambua ni Dylan hata niliposikia wamemwita Abdul nilisema poa tu lakini akija kwangu nitamwita ninalolitaka mimi kwa sababu nataka aitwe DD (D Square).”
Amesema alisikitishwa pia na kitendo cha mwanamke huyo kumualika baba yake katika sherehe ya kutimiza siku arobaini ya mtoto huyo akimdanganya kuwa angekuwepo.
“Walimwalika mzee Abdul na nguo wakampelekea ili ahudhurie, yote hiyo ili mradi tu wapate cha kuzungumziwa mitandaoni,” amesema.
Post a Comment
Powered by Blogger.