MAFUNZO YA ELIMU YA UFUNDI INANAFASI KUBWA YA KUKUZA AJIRA-RUTAYUGA

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakati wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Unesco ya kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.
 Afisa  Kiongozi wa UNESCO Dar es Salaam, Alex Plante akizungumza washiriki wa warsha ya kuzindua Mradi wa mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. 

 Baadhi ya washririki wa Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa UNESCO Dar es Salaam, Alex Plante,na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga wakiwa katika picha ya pamoja na  washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa  kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.


Na Karama Kenyunko, Glogu ya  jamii  
 MAFUNZO ya elimu ya ufundi yananafasi kubwa ya kuongeza, kusaidia  na kukuza ajira kwa vijana wanaosoma masomo hayo kwenye vyuo vya ufundi  kwa kuajiriwa au kujitengenezea ajira wao wenyewe.

Kaimu katibu mtendaji wa baraza la taifa elimu ya ufundi (Nacte), Dkt, Adolph Rutayuga amesema hayo jijini dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya mradi wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia,Dkt,Rutayuga amesema nia kubwa ya mradi huo ni kuangalia ufundi unaumuhimu gani kwenye sekta ya uchumi hasa unapozungumzia sekta ya uchumi wa viwanda.

Aidha tunaangalia ubora wa mafunzo yanayotolewa kwenye elimu ya ufundi sababu kukiwa na vyuo vingi ambavyo vinaendeshwa katika ubora usiotakiwa, wanafunzi wanaotoka kwenye vyuo hivi hawatakuwa wazuri.

“Tunalenga kujenga mazingira ya kutoa mafunzo bora kwenye elimu ya ufundi, elimu iliyobora kwa kusapoti walimu wanaofundisha,miundombinu ya kujifunza na kufundishia na pia kujaribu kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya viwanda na soko la ajira kwa kile kinachotolewa kwenye vyuo vya ufundi.

Ameongeza,kama suala zima la mambo ya mitaala, linaweza kuboreshwa, na ile dhana potufu ya kizamani iliyokuwepo kwamba kwamba Tivet ni kwa wale walioshindwa,inapaswa iondoke, watu wajue kwamba mchango mkubwa kwenye uchumi unafanywa na hawa watu kwenye sekta ya kati

“Malengo makubwa ni kujaribu kuinua ubora wa mafunzo yanayotolewa na vyuo vya ufundi, kuinua umuhimu  mafunzo ya ufundi na Jinsi inavyoweza kisaidia kwenye maendeleo ya kukuza uchumi”,amesema.

Naye, Afisa kiongozi wa Unesco nchini Axel Plathe amesema warsha hiyo itajadili kwa undani vitendo vya ufanisi, utekelezaji na jukumu la uwezo ambao kila wadau watafanya katika mradi uliopendekezwa chini ya maeneo matatu umuhimu, ubora na mtazamo wa elimu na ujuzi wa kiufundi.


“Elimu bora kwa Afrika itatekelezwa kuanzia mwaka huu hadi 2021 kwa lengo la kukuza elimu na ujuzi wa kitaaluma na mafunzo ambayo ni muhimu kwa mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya watu binafsi na jamii”amesema Plathe.
Post a Comment
Powered by Blogger.