KIWANDA CHA KUSINDIKA TUMBAKU SONAMCU KUFUFULIWA MKOANI RUVUMA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt.Binilith Mahenge amewahakikishia wananchi wa mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla kwamba mpango wa kufufua kiwanda cha kusindika tumbaku cha Songea na Namtumbo (SONAMCU) mkoani humo kilichokufa tangu mwaka 2002 unaendelea vizuri kwa kushirikiana na mwekezaji kampuni ya Premier ambapo kwa sasa inafanyika tathmini ya mitambo itakayotumika.

Akiongea katika jukwaa la maendeleo ya ushirika la mkoa wa Ruvuma, lililofanyika katika wilaya ya Tunduru, mkuu huyo wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge amesema kufufuliwa kwa kiwanda hicho cha kusindika Tumbaku cha SONAMCU kutafungua fursa za ajira zaidi ya 1,000 kwa wakazi wa Songea na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla na kwamba kinachofanyika sasa ni tathimini ya kuweka mitambo itakayotumika.

 Pamoja na serikali kuwa na jitihada mbalimbali za kunufaisha wananchi kupitia ushirika lakini ipo changamoto nyingine kubwa ya baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na siasa kufanya mipango na walanguzi ya kuwalaghai wakulima mazao yao kipindi cha mauzo.

Wakati huo huo, mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge amemuagiza kaimu katibu tawala wa mkoa huo, Bw. Biseko Bwai kumpa maeleo ya kwanini wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani humo ambao ndiyo wasimamizi wakuu wa ushirika wameshindwa kuhudhuria jukwaa hilo la maendeleo ya ushirika mkoa wa Ruvuma.

Chanzo: ITV Tanzania
Post a Comment
Powered by Blogger.