Watu wawili wamefariki katika matukio tofauti Mkoani Singida.

Watu  wawili   mkoani Singida wameuwawa  katika matukio mawili tofauti  likiwemo la jambazi  kuuwawa na polisi wakati wakirushiana risasi , na tukio lingine mtu mmoja kusukumwa  na kuangukia nje  katika  basi dogo lililokuwa katika mwendo wakasi.
Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida Mrakibu mwandamizi wa polisi Stella Mutabihirwa ,amesema  jambazi aliye tambulika kwa jina la  Salumu Issa amekufa wakati akipelekwa hospitali  baada ya  kupigwa risasi  na askari  ambaye yeye pia askari  ilimpiga kwanza risasi na jambazi wakati alipokuwa akitaka  kutoroka.
Katika tukio la pili kamanda Mutabihirwa amesema jeshi la polisi  lina mshikilia  Shabani  Mnghwira  utingo  wa basi dogo aina ya hice lenye usajili wa namba T.544 DFS, lililo kuwa likitokea  Singida kwenda Igunga mkoani Tabora  kumpiga kibao abiria moja mvulana  kisha kumsukumia nje na kuangukia kisogo kwenye  barabara ya lami na kupoteza maisha kwa madai ya kufunga mlango wa gari kwa nguvu.

Tukio la jambazi  kuuwawa limetokea katika kijiji cha Mukulu kata ya Mughunga wilayani Singida na askari kufanikiwa  kukamata  bastola  iliyotengenezwa kienyeji ikiwa na risasi ishirini na sita,tukio  lingine la  utingo kumsumkuma abiria  kutoka kwenye gari ambalo likiwa katika mwendo hadi nje ya barabara kisha kupoteza maisha limetokea katika kijiji cha Mseko kata ya Sheluhi wilayani Iramba.
Post a Comment
Powered by Blogger.