Rais Magufuli amfungulia mlango Mrisho Mpoto kwa Rais Museveni wa Uganda

Mrisho Mpoto akitambulishwa kwa Rais Museveni

Rais Magufuli wa Tanzania na Rais Yoweri Museveni alikuwa na zoezi la uweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa bomba la mafuta eneo la Chongoleani, Tanga ambapo tukio hilo lilihudhuriwa na wasanii wabongofleva kupata nafasi ya kupanda jukwaani na kuimba kisha raisi kuwaita kwa ajli ya kuwashika mkono.

Mshairi huyo ameonyesha furaha yake ya kukutanishwa na Rais Museveni wa Uganda na kudai nafasi hiyo nimfungulia milango mipya ya kibishara ndani ya nchi ya Uganda.

“Kila upatapo nafasi ya kumwambia Mungu asante fanya hivyo. Leo Mh Rais Magufuli kwa mapenzi yake akifanya utambulisho rasmi kwa Rais Uganda, “huyu ni Mzalendo anatusidia kujenga nchi tunaweza kumuazima kidogo lakini usimuibe” ni maneno ya faraja kutoka kwa mkuu wa nchi,” alindika Mpoto kupitia Instagram.

Mpoto ameonekana kuwa karibu zaidi na Rais Magufuli kutokana na kufanya kazi nyingi za Ikulu kwa ukaribu hali zaidi kushinda wasanii wengine.

Mshairi huyo hivi karibuni alinukuliwa na kituo kimoja cha redio kwamba anaonekana kuwa karibu zaidi na Rais Magufuki kutokana na kazi zake za muziki hasa hasa zile ambazo zinazungumzia uzalendo zaidi na sio mambo mengine
Post a Comment
Powered by Blogger.