GHOROFA REFU DUNIANI LA MAKAZI YA WATU LAUNGUA MOTO DUBAI


Ghorofa lenye urefu wa futi 1,100 nchini Dubai limeungua moto upande mmoja leo afajiri katika tukio ambalo hata hivyo wakazi wake wote wametoka salama.Moto huo ulisambaa kwa kasi katika ghorofa hilo la makazi ya watu lililorefu zaidi kuliko yote duniani na kusababisha mtafaruku kwa wakazi wake huku kukiwa na joto la 45c.Picha za video zinaonyesha jinsi moto huo ulivyokuwa unapanda juu katika ghorofa hilo lenye ghorofa 86, huku sehemu ya moto ukiangukia gari zilizoegesha chini.
                                 Ghorofa refu la makazi Dubai likiwa linawaka moto leo alfajiri

Magari yaliyokuwa yameegeshwa chini ya ghorofa hiyo yakiwa yameathiriwa na moto huo
Watu wakiangalia moto uliokuwa ukiunguza ghorofa la makazi Dubai hata hivyo moto huo ulidhibitiwa.

Post a Comment
Powered by Blogger.